Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

WATALAAM wa afya kutoka nchi za Asia Pacifc na Afrika wamekutana leo kwenye madahalo wa pili wa kujadili na kubadilisha uzoefu katika kupambana na virusi vya Corona.

Mdahalo huo umefanyika kupitia Kituo cha Mafunzo duniani (TaGLC) kilicho chini ya Chuo cha Utumishi wa Umma (TPSC) kwa kushirikiana na GDLN, Korea.
Kwa mara ya kwanza mdahalo wa aina hiyo uliofanyika Machi 16, mwaka 2020 na kwa sehemu kubwa ulijikita kuhusu athari na jinsi ya kupambana na Virusi vya Corona (COVID 19).

Katika mdahalo wa leo watalaam kutoka Asia Pacific (Korea, Hong Kong, Sri Lanka, Singapore, Australia) na Tanzania wamewasilisha uzoefu wa nchi zao katika kupambana na virusi vya CORONA na athari zake.

Taarifa iliyotolewa leo Aprili 2 mwaka 2020 kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam imesema kuwa wasemaji wakuu katika mdahalo huo walikuwa Dk.Sapumal Dhanapala wa Shirika la Afya Sri Lanka, Profesa Kamalini Lokuge kutoka Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Australia, Dk. Jayant Menon, (ISEAS / ADB) kutoka Singapore na Dk.Janeth Mghamba & Dr. Joseph Hokororo.

Kwa Tanzania Wajumbe wa Kikosi cha Kitaifa kukabilina na virusi vya Corona ( COVID 19) waliwasilisha maada wakati wa kikao kuhusu uzoefu wa nchi zao. Mazungumzo yalisimamiwa na Profesa Hai - Young Yun kutoka Taasisi ya Elimu ya KDI, Korea.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa ujumla wataalamu hao walishirikishana uzoefu katika maeneo ya Uanzishaji vituo vya upimaji wa uchunguzi wa
Kitabibu wa Virusi vya COVID, kusimamia na kuzuia milipuko/maambukizi Mapya , athari za kiuchumi zitokanazo na COVID -19, kulinda huduma muhimu za afya zisizohusu COVID 19, na miongozo ya afya za msingi kuhusu kuzuia mambukizi.

Hata hivyo washiriki walihudhuria mdahalo huo kupitia mtandao (online streaming) na wengine wachache walishiriki kupitia ofisi za TaGLC zilizopo katika Mtaa wa Shabaan Robert, Jengo la IFM ambapo tahadhali zote dhidi ya maabukizi zilichukuliwa.
Mkurugenzi Msaidizi, Kitengo na Udhibiti wa Magonjwa ya mlipuko, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Janneth Mghamba (kushoto) kizungumza na Michuzi Tv baada ya kumalizika mdahalo wa kimataifa kwa njia ya video kuhusu kukabiliana na virusi vya corona (COVID 19) na athari za kuenea kwake. Mkutano huo uliandaliwa na Kituo Cha Mafunzo cha Kimataifa (TaGLC) kwa kushirikiana na GDLN, Korea leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kituo.Bw. Brown Hasunga.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kimataifa (TaGLC).Bw.Brown Hasunga (kulia)akisisitiza jambo wakati wa mdahalo wa kimataifa kwa njia ya video kuhusu kukabiliana na virusi vya corona (covid – 19) na athari za kuenea kwake. leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Wadau mbalimbali wa Afya pamoja na watumishi wa Kituo Cha Mafunzo cha Kimataifa (TaGLC) wakimsikiliza mtoa mada kwa njia ya video katika mdahalo wa kimataifa kwa njia ya video kuhusu kukabiliana na virusi vya corona (COVID 19) na athari za kuenea kwake. Mkutano huo uliandaliwa na Kituo Cha Mafunzo cha Kimataifa (TaGLC) kwa kushirikiana na GDLN, Korea leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...