Na Farida Saidy,Morogoro
Baraza
la Makanisa ya Pentekoste Tanzania (CPCT) Mkoa wa Morogoro wameungana
na jitihada za Serikali ya Mkoa huo kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni
moja za kitanzania ikiwa ni mchango wao katika kupambana na ugonjwa wa
CORONA Mkoani humo.
Viongozi
wa CPCT wametoa msaada huo wa fedha mwishoni mwa wiki hii walipofika
ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kumkabidhi fedha hizo Mkuu wa
Mkoa huo Loata Ole Sanare kama ishara ya kumuunga Mkono na Serikali
ngazi ya Mkoa katika kupambana na ugonjwa wa CORONA Mkoani humo.
Wakizungumzia
mara baada ya kutoa msaada huo, Viongozi wa CPCT wakiongozwa na Askofu
Bryson Msuya Askofu wa TAG Morogoro Kaskazini ambaye pia ndiye
Mwenyekiti wa CPCT Mkoa wa Morogoro walieleza kuwa wameguswa na jitihada
za Mkuu wa Mkoa za kupambana na ugonjwa wa CORONA.
Hamasa
ya viongozi hao inatokana na wito alioutoa Mkuu wa Mkoa huo Loata
Sanare Aprili 21 mwaka huu katika kikao chake na wadau mbalimbali wa
maendeleo Mkoani humo kilichofanyika katika Chuo cha ualimu cha
Morogoro ambapo kwa pamoja walikubaliana kuunganisha nguvu zao ili
kupambana na janga la CORONA ambalo bado ni tishio kwa Taifa la Tanzania
na Dunia kwa jumla.
Akipokea
mchango huo Loata Ole Sanare aliwashukuru viongozi hao kwa mchango
walioutoa huku akisisitiza kauli yake anayoitoa mara kwa mara kuwa
pamoja na michango ambayo ni muhimu, kubwa aliwataka viongozi hao kutoa
elimu kwa watu wanaowahudumia katika maeneo yao namna ya kujikinga na
maambukizi ya CORONA.
Aprili
24 mwaka huu yaani siku tatu baada ya kikao cha Mkuu wa Mkoa na wadau
kufanyika, michango mbalimbali ilianza kumiminika Ofisini kwa Mkuu wa
Mkoa kutoka kwa wadau ikiwa ni utekelezaji wa ahadi walizotoa siku ya
kikao ambapo siku hiyo pekee vifaa na fedha taslimu vilipatikana, vyote
vikiwa na jumla ya zaidi ya shilingi 141Mil.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare (kushoto) akipokea msaada wa
shilingi milioni moja kutoka kwa mwakilishi wa Viongozi wa Baraza la
Makanisa ya Pentekoste Tanzania Mkoani Morogoro Askofu Brayson Msuya
ambaye pia ni Mwenyekiti wa CPCT Morogoro (picha - Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...