Na Woinde Shizza,Arusha
Uongozi
wa bar maarufu ya picnic iliyopo katikati ya jiji la Arusha umeelezea
mikakati mbalimbali ambayo wanaitekeleza kipindi hiki katika kupambana
na janga la ugonjwa hatari wa Corona.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa bar hiyo, Bodia Kaaya alisema kwamba
kufuatia janga la corona wao kama watoa huduma wamechukua hatua
mbalimbali ikiwemo kuhakikisha wahudumu wao wanavaa barakoa muda wote
wakati wa kutoa huduma.
Kaaya,alisema
kwamba mbali na barakoa pia wamehakikisha wameweka ndoo za maji na
sabuni katika milango ya kuingilia ndani ya eneo lao ili kunawa mikono
yao kabla hawajaingia kupata huduma.
Alisema
kwamba wametoa vitakasa mikono lakini pia wanapulizia dawa katika meza
mbalimbali zilizopo ndani ya eneo lao kama njia mojawapo ya kupambana na
corona.
Pia alisisitiza
wanafuata kanuni zote zilizotolewa na wizara ya afya nchini ambapo
wanawafundisha watumishi wao namna ya kuchukua tahadhari na ugonjwa wa
corona.
"Tunachukua
tahadhari zote tunazoelekezwa na wizara ya afya lakini pia
tunawafundisha wafanyakazi wetu namna ya kujikinga na gonjwa
hili"alisema meneja huyo
Naye
mtumishi wa bar hiyo,Elisante Charles alisema kwamba wao kama watumishi
wameelekezwa hatua zote za kuchukua kujikinga na gonjwa la corona kama
kuvaa barakoa muda wote wawapo kazini.
Charles,
alisema kwamba baadhi ya watumishi wa afya wamekuwa wakipita mara kwa
Mara katika bar hiyo na kuwapa elimu mbalimbali na kufanya ukaguzi na
kuiomba serikali kufanya hivyo kwenye maeneo mengine
"Witumishi
wa idara ya Afya hapa Arusha wametupatia semina ya kutosha namna ya
kujikinga na corona wakati wa kutoa huduma pia vifaa vipo vya kutosha
uongozi umezingatia hilo na kufanya kazi kuwa rahisi alisema Charles.
Pichani ni Meneja wa Bar ya Picnic, Bodia Kaaya akisafisha meza kwa kutumia dawa kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona (covid 19).
Picha meneja wa bar ya Picnic akimwagia mteja sabuni anawe mikono kabla ya kuingia Ndani ya bar hiyo kupata huduma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...