Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
BRAZIL
ni nchi kubwa katika bara la Amerika ya Kusini, huku jina la nchi hiyo
ikitokana na mti uliojulikana 'Brazilwood' kireno inaitwa Brasil ambayo
ni lugha rasmi nchini humo, Brazil ni nchi pekee inayozungumza Kireno
Amerika Kusini huku ikiwa na watu zaidi ya milioni 200 na imepakana na
nchi zote za Amerika Kusini isipokuwa Chile na Ecuador.
Brazil
ilikuwa koloni ka wareno kwa miaka 322 kabla ya kupata uhuru wake 1822,
na imekua nchi ya mwisho kabisa kukomesha biashara ya utumwa mwaka 1888
huko Amerika, pia Brazil ni nchi ya tano kwa ukubwa duniani
kijiografia na kwa idadi ya watu, Mji mkuu wa Brazil ni Brasilia na mji
mkubwa zaidi ni Sao Paulo huku miji mikubwa ikiwa Rio de Janeiro,
Salvador na Fortaleza.
Ikiwa
moja ya nchi yenye uchumi mkubwa Brazil inafanya shughuli mbalimbali
ikiwemo kilimo hasa kahawa zao ambalo linazalishwa kwa wingi nchini humo
tangu miaka 150 iliyopita, uchimbaji madini, uvuvi pamoja na shughuli
za utalii ambapo kwa mwaka watalii zaidi ya milioni 6 hutembelea nchi
hiyo lakini bado wanakumbana na matatizo kama umaskini, kutokuwa na
usawa, changamoto za kiutawala na mazingira.
Brazil
ina jumla ya viwanja vya ndege zaidi ya 700 katika miji 639, pamoja na
hazina kubwa ya mto wa Amazon ambao ni wa pili kiukubwa duniani
ukitanguliwa na mto Nile na hiyo ni pamoja na wanyama wa kipekee
wakiwemo jaguars na pumas.
Brazil
pia ipo vizuri katika sekta ya michezo, timu ya taifa ya mpira wa miguu
nchini humo ni moja kati ya timu bora zaidi duniani na imetwaa kombe la
dunia mara tano huku ikiwa na wachezaji maarufu kama Neymar, Ronaldo na
Anderson Silva.
Tukio
kubwa lililovunja rekodi kwa mujibu wa Guinness Book of World Records ni
lile la Agosti 6-7, 2006 ambapo kikundi cha watu 10 kilivamia benki na
kuiba fedha zipatazo dola za kimarekani 70 milioni katika mji wa
Fortaleza.
Pia katika
mji wa Sao Paulo umetajwa kuwa eneo lenye foleni zaidi (Traffic jam)
hasa nyakati za jioni, imewahi kurekodiwa kuwa na foleni kwa kilometa
309 kwa mwaka 2013.
Jardim Gramacho ni dampo kubwa duniani lililogundulika katika mji wa Duque de Caxias nchini humo na lilifungwa mwaka 2012.
Licha ya hayo Brazil ina upekee wa jumla ya vivutio 72 ikiwa inaongoza kwa kuwa na vivutio vingi katika bara la Amerika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...