USALAMA KATIKA SIKUKUU YA EID EL FITR.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa
kuimarisha ulinzi na usalama katika kipindi chote cha kusherehekea sikukuu ya EID
EL FITR na hakuna tukio kubwa la uhalifu lililoripotiwa kutokea. Aidha
wananchi wamesherehekea kwa Amani na Utulivu huku wakiendelea kuchukua
tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa hatari wa Homa Kali ya Mapafu [COVID
19].
KUKAMATWA
KWA WATUHUMIWA SUGU WA MATUKIO YA UVUNJAJI.
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili [02] 1. KELVIN THOMAS
[32] Mkazi wa Mwakibete na 2. SAID KIBIKI [30] Mkazi wa VETA –
Ilomba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uvunjaji na wizi wa mali
mbalimbali.
Watuhumiwa
wamekamatwa katika msako uliofanyika kuanzia tarehe 22.05.2020 hadi
26.05.2020 katika maeneo ya Mwakibete, VETA na Pambogo Jijini Mbeya na
kufanikiwa kuwakuta na mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
1. Flat Screen
nne [04] za aina mbalimbali.
2. Radio
Sub-Woofer nane [08] za aina mbalimbali
3. Monitor nne
[04] na CPU mbili [02] za Kompyuta.
4. Amplifier
kubwa mbili [02]
5. Equalizer
moja [01]
6. Hard Disk
moja [01]
7. Spika kumi
[10] za aina mbalimbali
8. Mtungi
mmoja wa Jiko la Gesi aina ya Oryx
9. Keyboard
nne [04] za Kompyuta
10. Deck moja
aina ya Singsung
11. Stabilizer
moja
12. Viatu Jozi
nne na Sandles za kiume Jozi moja
13. Vifaa
mbalimbali vya kuvunjia.
Jeshi la
Polisi linatoa wito kwa mtu yeyote aliyeibiwa vitu vyake kufika Kituo Kikuu cha
Polisi Mbeya [Central Police Station] kwa ajili ya utambuzi wa mali hizo.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa
watafikishwa mahakamani.
KUJERUHI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa nane
[08] kutokana na tuhuma za kushiriki kwenye tukio la kujeruhi baada ya
kutokea ugomvi kati ya raia wa China wanaomiliki kampuni ya michezo ya
kubahatisha “BONANZA” na watu waliokuwa wanacheza mchezo huo.
Ni kwamba mnamo tarehe 25.05.2020 majira ya saa
16:00 jioni huko maeneo ya Soweto, Kata ya Ruanda, Tarafa ya Iyunga, Jiji
la Mbeya. Watu wawili ambao ni ABISON HAMISI [36] na GILBERT
MWAKANYEMBA [32] Mjasiliamali wote wakazi wa Manga Veta walijeruhiwa kwa
kukatwa panga [sime] sehemu mbalimbali za miili yao na raia wa China kwa
kushirikiana na baadhi ya wafanyakazi wao wa kampuni ya michezo ya kubahatisha
ya Bonanza.
Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliozuka kati ya CHEN YEN
[43] mfanyabiashara, raia wa China, mkazi wa Veta na ABISON HAMIS @ NDELE
baada ya ABISON kutamka neno la kichina lililomuudhi CHEN YEN na
kusababisha ugomvi uliopelekea baadhi ya watu kujeruhiwa.
Awali raia huyo wa China alifika eneo hilo kuchukua fedha
kwenye mashine ya mchezo wa kubahatisha ya kampuni ya Bonanza akiwa amefuatana
na dereva wake GIFT ELIA @ MWAMELO [23] mkazi wa Airport wakiwa na Gari T.
252 DNL Toyota Kluger katika eneo lijulikanalo "Sports
Centre" linalomilikiwa na SALUM JUMA. Aidha ABISON HAMIS
alifika kucheza Pool akiwa ameongozana na GILBERT MWAKANYEMBA na KENEDY
MWAMLIMA na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la YOHANA.
Kufuatia tukio hilo raia huyo wa China alipiga simu kuomba
msaada kwa wenzake ambao ni raia wa China ndipo walifika na kuanza
kuwashumbulia ABISON HAMIS @ NDELE na GILBERT MWAKANGEMBA
kwa sime maeneo mbalimbali ya miili yao. Aidha ABISON HAMIS @ NDELE
na GILBERT MWAKANYEMBA wamelazwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya
wakiendelea kupatiwa matibabu.
Pia kufuatia vurugu hizo Gari namba T.252 DNL Toyota
Kluger liliharibiwa vibaya kwa kuvunjwa vioo vyote na wananchi wa eneo hilo
waliokuwa wakiwashambulia wachina ili kuwaokoa ABISON HAMIS @ NDELE na
GILBERT MWAKANYEMBA na upotevu wa mali zikiwemo fedha Tshs 3,000,000,
simu ya mkononi aina ya Iphone.
Kutokana na tukio hilo msako mkali umefanyika na watu 8 wamekamatwa
ambao ni 1. CHEN YEN [43] mfanyabiashara na mkazi wa Meta, 2.
XIAO JING [30] mfanyabiashara na mkazi wa Meta, 3. LIN HAI
[30] mfanyabiashara na mkazi wa Meta, 4. LYU JIAN QZING [36]
mfanyabiashara na mkazi wa meta, 5. JIANG ZE DONG [39]
mfanyabiashara na mkazi wa Meta, 6. GIFT ELIA [23] dereva na
mkazi wa Airport, 7. HERMAN ELIAS @ MWALWIBA [20] dereva na mkazi
wa Esso na 8. KENED MWAMLIMA [28] dereva, mkazi wa Ituha.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 24.05.2020 majira ya saa 23:30 usiku
huko Kitongoji cha Matundasi “A”, Kata ya Matundasi, Tarafa ya Kiwanja,
Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya.
tulimkamata RICHARD BONIFACE [31] Mkazi wa Matundasi “A” akiwa na
bhangi gramu 245. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa bhangi.
Imetolewa
na:
[ULRICH
O. MATEI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...