Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), Wameendelea kurudisha fadhila kwa wateja wao na jamii kwa ujumla kwa kujenga Vizimba Vingine viwili vya kunawia mikono, ikiwa ni tahadhari ya kujikinga gonjwa la corona,na hivyo kufanya Idadi ya vizimba hivyo kufikia vitano vilivyojengwa ndani ya Manispaa ya Bukoba.

Akisoma Taarifa ya utelekezaji wa miradi hiyo, Mkurugenzi wa BUWASA Ndg. John Sirati amesema kuwa Mamlaka katika kuhakikisha jamii inaendelea kuchukua Tahadhari ya Corona, wamendelea kujenga Vizimba vingine viwili vya kunawia mikono kimoja kikijengwa Kituo Kikuu cha Polisi, na Kingine katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Bukoba, na kufanya Idadi ya Vizimba kufikia vitano huku Vizimba kama hivyo vikiwa tayari vimejengwa Stendi kuu na Stendi ya dharula na Soko kuu la Bukoba.

Akizindua Vizimba hivyo, Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa Kagera, Profesa Faustine Kamuzora amewataka Wananchi wanaofika maeneo hayo kuendelea kunawa mikono kwani kwa kufanya hivyo, ni kinga ya magonjwa mbalimbali na Corona ikiwa miongoni, na kwamba kunawa mikono na kuchukua tahadhali kutasaidia kujikinga na kuwakinga wengine.

Aidha Profesa Kamuzora amewashukuru BUWASA kwa kuona umuhimu wa kurudisha fadhila kwa wananchi, na kuwaomba wasichoke pale wanapoona kuna uhitaji, huku akisisitiza juu ya huduma zitolewazo na BUWASA huku akidai kuwa wamejitahidi kutoa huduma nzuri hasa kutokatika Maji wakati wote.
Pichani ni Katibu Tawala Mkoa Kagera Profesa Faustine Kamuzora akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kizimba kipya cha kunawia Mikono eneo la Hospitali ya Rufaa Bukoba, kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa BUWASA Ndg. John Sirati, na kulia ni Muuguzi mfawidhi wa Hospitali Sr. Mariagoleth Rusangiza.
 Pichani ni Kaimu Katibu wa Hospitali ya Rufaa Bukoba Bi. Deodatha Mugisha akizungumza na wanahabari Mara baada ya kupokea kizimba hicho, kubwa akitoa shukrani zake na kuahidi kutunza kizimba hicho kwa manufaa ya Wananchi.
 Pichani anaonekan Mkurugenzi Mtendaji wa BUWASA Ndg John Sirati akisoma taarifa ya Miradi iliyotekelezwa na BUWASA ambayo ni Vizimba Vitano na Ndoo 30 za kunawia Mikono vyenye thamani zaidi ya Shilingi Milioni Sita.
 Pichani anaonekana Mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Bukoba, akinawa mikono katika kizimba kipya cha kunawia mikono kilichojengwa na BUWASA lengo ikiwa Wananchi waendelea kuchukua Tahadhari ya Ugonjwa wa Corona
 Pichani ni Muonekano wa kizimba kimojawapo kilichojengwa na BUWASA eneo la Hospitali ya Rufaa Bukoba, ikiwa ni kati ya Vizimba vitano vyenye muonekano huo, kila kimoja kikiwa na thamani ya Milioni moja na Nusu.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...