Na Shukrani Kawogo, Njombe
Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)wilayani Ludewa mkoani Njombe imeishauri serikali kupitia mkuu wa wilaya hiyo Adrea Tsere kuweka mkakati madhubuti wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (COVID 19) katika maeneo ya mikusanyiko ikiwemo maeneo ya minada na maeneo ya kuingilia ndani ya wilaya.
Ushauri huo umetolewa katika kikao cha taarifa juu ya mwenendo wa ugonjwa huo katika wilaya hiyo ambayo ilitolewa na Muuguzi mkuu ofisi ya wilaya Bw. Cyprian Mgaya ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa hakuna mshukiwa wala mgonjwa aliyepatikana na ugonjwa huo.
Alisema kuwa pamoja na kwamba hakuna mshukiwa wala mgonjwa yeyote lakini bado wanafanya juhudi ya kutoa elimu kwa watu pia kuweka mazingira mazuri ya kujikinga na ugonjwa huo.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya Bw. Stanley Kolimba alisema kuwa katika maeneo ya minada kumekuwa na muingiliano wa watu hivyo ofisi ya wilaya inapaswa kuhakikisha kuwa katika kila lango la kuingilia mnadani kunawekwa maji tiririka pamoja na vitakasa mikono na awepo mtu atakayesimamia zoezi hilo.
Aliongeza kuwa kwa muingiliano huo mkubwa wa watu ni rahisi kuenea kwa maambukizi hivyo ikiwezekana kila mfanyabiashara aliyepo katika eneo hilo la mnada aweke maji tiririka katika eneo la biashara yake na mteja atakapofika kwenye biashara yake anawe mikono kwanza.
Aidha kwa upande wa katibu wa Chama hicho Bakari Mfaume amesema kuwa pamoja na kuweka mikakati hiyo katika maeneo ya minada pia katika maeneo ya kuingilia wilayani humo kuwepo na wataalamu wa afya kwa ajili ya kuwapima watu wanaoingia wilayani humo.
“Watu wote watakao ingia kupitia mipaka yote ya wilaya hiyo kuwepo utaratibu wa kuwapima kwa kutumia kipima joto ili kuona kama wanaweza kupata washukiwa wa ugonjwa huo na kujiridhisha kuwa watu wanaoingia wilayani kwetu wapo salama”. Alisema Mfaume.
Hata hivyo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya muungano Tanzani Dk. John Pombe Magufuli kwa juhudi na msimamo wake juu ya mikakati ya udhibiti wa ugonjwa huo wamemuelewa na wameona faida yake.

Kutoka Kushoto Mwenyekiti CCM Ludewa Stanley Kolimba, Katibu CCM Ludewa Bakari Mfaume na Muuguzi mkuu wilaya ya Ludewa Cyprian Mgaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...