Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WENGI
hufikiri kuwa kuzaliwa kawaida ni kawaida, ila kwa Claudio Viera de
Oliveira ni tofauti kabisa, yeye amezaliwa kichwa kikiwa kimeangalia juu
pamoja na ulemavu wa mikono na miguu,na alipozaliwa madaktari
walimshauri mama yake Maria Jose Vieira amuache Claudio afe kwani
angemsumbua mno katika malezi lakini mama yake alipuuzia ushauri huo.
Licha
ya ulemavu huo Claudio hakukata tamaa, akiwa na miaka 40 aliweza
kuandika kitabu kilichohusu maisha yake kiitwacho 'Omundo Esta Ao
Contrario:
Claudio raia
wa Brazil alizaliwa na tatizo hilo ambalo hutokea mara chache sana,
kitaalamu linajulikama kama 'arthrogryposis' hali ya misuli katika
sehemu ya mwili kushindwa kujikunja na kujikunjua na kubaki ikiwa
imekakamaa.
Claudio
alianza kujifunza kuandika kwa kutumia mdomo ili aweze kupambana na
changamoto iliyokuwa ikimkabili na aliweza kutimiza ndoto yake ya kuwa
mhasibu pamoja na kutoa mihadhara katika matukio mbalimbali.
Akiwa
na miaka 40 alichapisha kitabu chake cha kwanza kiitwacho 'Omundo Esta
Ao Contrario' ambacho kimeelezea maisha yake na uzoefu alioupata
kupitia hali yake pamoja na mchango wa mama yake katika kufikia malengo.
Mama
wa kijana huyo amewahi kueleza vyombo vya habari kuwa alishauriwa na
madaktari kumwacha kijana wake afariki dunia kwa kuwa asingeweza kupumua
vizuri na wengine walimshauri asimpe chakula lakini hakusikiliza
ushauri huo.
"Alianza
kutembea mwenyewe baada ya kubebwa kila mahali kwa miaka nane na
alijifunza kufanya vitu kama watu wengine bila kuhitaji msaada, mwanangu
anajiamini sana ninajivunia" alieleza mama huyo.
Claudio
amenukuliwa akieleza kuwa tangu alipokuwa mtoto hakupenda kuwategemea
watu wengine daima alikuwa akijishughulisha na kazi na amekuwa
akijifunza kupitia televisheni, simu, redio pamoja na mitandao
mbalimbali hadi akatimiza ndoto na kutunukiwa shahada ya uhasibu katika
chuo kikuu cha Feira de Santana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...