Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa
Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu amekagua ujenzi nyumba ya Mwalimu huku
Wakazi wa Kijiji cha Mpunda kilichopo kata ya Michenjele wakimshukuru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwajengea nyumba ya kuishi
Mwalimu katika shule ya msingi Mpunda.
"Tunamshuru
Rais Magufuli kutuletea fedha za kujenga nyumba hii ya Mwalimu.
Haijawahi kutokea tangu tupate Uhuru maendeleo haya ya kasi tunayoyaona.
Pia tunamshukuru Afisa Tarafa Mihambwe kututembelea mara kwa mara kujua
maendeleo ya mradi huu." alisema Mzee Issa Mohammed Mnindanga (65)
Naye Mwalimu wa shule hiyo alimshukuru Rais Magufuli kuwapunguzia kero ya makazi ya kuishi mbali.
"Namshukuru
sana Rais wetu John Pombe Magufuli kutupunguzia kero ya makazi sisi
Waalimu. Tunampenda na tunamwahidi ushirikiano nae." Alisema Mwalimu
Flower Valentine Kibombo wa shule ya msingi Mpunda.
Gavana
Shilatu aliwasisitiza kamati kuwa Makini na mradi huu wa ujenzi na
mafundi kujenga kwa kasi na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha.
"Nami
naungana na Wananchi hawa kumshukuru Rais Magufuli kutuletea fedha Tsh
milioni ishirini na tano (25,000,000/=) za kujenga nyumba ya Kwanza
kabisa ya Mwalimu kijijini hapa tangu tupate Uhuru. Kuhusu ujenzi
sipendi kusikia fundi unachakachua mradi na kamati ihakikishe inapokea
vifaa vyote toka kwa Mzabuni kama ambavyo vimeainishwa kwenye BOQ. Muwe
wakali na huu mradi ukamilike." Alisisitiza Gavana Shilatu wakati
akiongea na Kamati ya ujenzi na uongozi wa shule.
"Kama
fundi ninahaidi kujenga kwa uaminifu na kwa ubora na vifaa
nitakavyokabidhiwa nitavitumia vyote pasipo kuvichakachua." Alisema
Fundi msimamizi Hamza Kaume.
Gavana
Shilatu alifanya ziara ya kikazi kukagua mradi huo wa ujenzi wa nyumba
ya Mwalimu ulioanza kwa nguvu ya Wananchi Tsh. Milioni nane na Rais
Magufuli kutoa fedha Tsh. Milioni ishirini na tano za kumalizia mradi
huo na kufanya gharama kuu za mradi huo kuwa Tsh. Milioni thelathini na
tatu. Mradi huo unatarajia kukabidhiwa rasmi mwezi Juni, 2020 tayari
kwa matumizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...