Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium mbele ya mkurugenzi wa Mji wa Mafinga.

Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium .

Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga.


NA MWANDISHI WETU,MUFINDI.

Baada ya kupokea mashuka 120 kutoka katika kampuni
ya Qwihaya General Enterprises Ltd, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium ameishukuru kampuni hiyo na kuwaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Covid 19.

Jana Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd,
Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Mbali na msaada huyo, kampuni hiyo imefanikiwa kuikabidhi Serikali ya mkoa wa Iringa, vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni yakiwemo mavazi 20 ya madaktari, matenki 60 ya kuhifadhia maji, barakoa na vitakasa mikono.

“Kipekee nimshukuru ndugu yetu Qwihaya kwa msaada huu, mashuka haya yatatusaidia, wito wangu kwa wadau wengine tuungane mkono ili tuweze wote kwa pamoja kulikabili janga hili,” amesema DC wa Mufindi.

Awali, Ndugu Mahenda alisema bado kuna vifaa vingine vimeandaliwa kwa ajili ya kuikabidhi wilaya hiyo katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

“Bado tuna vifaa ambavyo tumeandaa kwa ajili ya halmashauri yetu ambavyo tutaleta kuendelea kukabiliana na ugonjwa huu, niwaombe wadau wengine waweze kujitokeza kukabiliana na ugonjwa huu,” amesema Mahenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...