Na Verediana Mgoma,Jimbo la Musoma Vijijini
KIJIJI cha BUANGA cha Kata ya RUSOLI kina Jumla ya VITONGOJI 9 na SHULE za MSINGI 2 (S/M Bwenda na S/M Bwenda B).
MWALIMU
MKUU wa S/M Bwenda B, Mwl Christopher Cosmas amesema Shule hiyo
iliyofunguliwa Mwaka 2015 ina jumla ya WANAFUNZI 482, VYUMBA vya
MADARASA 4 na inao UPUNGUFU wa Vyumba 5 vya Madarasa. Kwa hiyo MADARASA 4
yanasomea CHINI ya MITI na kipo Chumba cha Darasa kina WANAFUNZI 99.
MATATIZO
ya UMBALI MREFU wa kutembea na MIRUNDIKANO madarasani ya WANAFUNZI wa
kutoka VITONGOJI 9 vya Kijiji cha Buanga, yamewalazimisha WANANCHI
WAAMUE kuyatatua kwa kujenga SHULE SHIKIZI MPYA kwenye KITONGOJI cha
CHIRUGWE.
MWENYEKITI wa
Kijiji cha Buanga, Ndugu Kejile Eyembe amesema WATOTO WAO wanatembea
umbali wa KILOMITA 5 kwenda masomoni kwenye Shule Mama ya Bwenda (S/M
Bwenda & S/M Bwenda B). Kwa hiyo, WAMEAMUA kujenga Shule MPYA, yaani
SHULE SHIKIZI na WANANCHI WAMEKUBALIANA kuchanga Tsh 10,000 (elfu kumi)
kutoka kila KAYA, na tayari ujenzi umeanza.
DIWANI
wa Kata ya RUSOLI, Mhe Boaz Nyeula amesema UJENZI wa SHULE hiyo
unachangiwa na NGUVUKAZI na FEDHA za WANAKIJIJI, na WADAU wengine wa
MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA wa Kijiji cha Buanga.
MALENGO ya UJENZI ni kukamilisha VYUMBA 7 vya MADARASA, OFISI 1 ya Walimu na VYOO vya Wanafunzi na Walimu.
SHUKRANI KUTOKA KIJIJI CHA BUANGA
Wananchi na Viongozi wa Kijiji cha Buanga wakiongozwa na Diwani wao huyo wanatoa SHUKRANI nyingi kwa:
*
SERIKALI na HALMASHAURI yake kwa kushirikiana na WANANCHI kujenga na
kuboresha MIUNDOMBINU ya Shule za Msingi za Kijiji cha Buanga na Kata
yao yote ya Rusoli.
* PLAN CONCERN INTERNATIONAL (PCI) kwa kujenga VYOO, kugawa VITABU na CHAKULA kwa Wanafunzi.
* MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo kwa MICHANGO yake ya:
(i) S/M Bwenda -
Madawati 92, Saruji Mifuko 60 na Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) S/M Bwenda B -
Madawati 70, Saruji Mifuko 60, Mabati 50 na Vitabu vingi vya Maktaba
(iii) Shule SHIKIZI inayojengwa: SARUJI MIFUKO 100.
OMBI KUTOKA KWA WANAKIJIJI
WAZALIWA
wa Kijiji cha Buanga na Kata ya RUSOLI wanaombwa WAJITOKEZE KUCHANGIA
UJENZI wa SHULE SHIKIZI ya Kijiji cha Buanga iliyopangwa kufunguliwa
mwakani (Januari 2021).
SHULE ZA MSINGI NDANI YA JIMBO LETU
HALMASHAURI ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) na JIMBO lake la Musoma Vijijini (Vijiji 68, Kata 21) ina jumla ya:
* Shule za Msingi za Serikali 111
* Shule za Msingi za Binafsi 3
* Shule Shikizi 11 (nyingine zimeishafunguliwa na nyingine zinakamilisha ujenzi)
* MAKTABA kwenye Shule za Msingi zipo chache na ujenzi unaendelea.
PICHA za hapa zinaonesha WANANCHI na VIONGOZI wao wa
Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli wakiendelea na UJENZI wa VYUMBA vya
MADARASA ya SHULE SHIKIZI yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...