RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amemtumia salamu za rambirambi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kufuatia kifo
cha Waziri wa Katiba na Sheria Balozi
Agostine Mahiga.
Balozi Mahiga alifariki nyumbani wake Mjini Dodoma
baada ya kuugua hafla ambapo alipofikishwa hospitali tayari alikwishapoteza
uhai na kuzikwa jana Mkoani Iringa.
Katika salamu hizo Dk. Shein alisema amepokea kwa
mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha Waziri wa Katiba na Sheria wa Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Agustine Mahiga kilichotokea Mjini Dodoma.
“Kwa niaba ya watu wa Zanzibar na Serikali natoa
mkono wa pole na rambirambi kwako Mheshimiwa Rais, familia ya marehemu pamoja
na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa msiba wa kuondokewa na
kiongozi aliyekuwa na upendo wa nchi yetu”, ilieleza sehemu ya salamu hizo za
rambirambi alizozituba Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alisema Balozi Mahiga ataendelea kukumbukwa kwa
mchango wake mkubwa katika kulinda na kutetea maslahi ya nchi katika shughuli
za kimataifa ikiwemo Afrika Mashariki, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na
taasisi nyengine.
Dk. Shein alisema kuwa Balozi Mahiga alikuwa
mstari wa mbele katika kuleta maendeleo na kudumisha umoja, amani na upendo
katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufuata misingi ya Katiba na Sheria.
Rais Dk. Shein alimuomba Mwenyezi Mungu awajaalie
wafiwa na wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania moyo wa subira
katika kipindi hichi cha msiba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...