************************************

Na Woinde Shizza , Arusha .

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro leo amezindua kiwanda kidogo kitakachokuwa kikizalisha Barakoa kwa ajili ya watumishi wa wilaya hiyo katika sekta ya afya. 

Akizindua kiwanda hicho kidogo cha uzalishaji wa barakoa katika wilaya hiyo kuwa hicho litasaidia kutengeneza barakoa kwaajili ya wafanyakazi wote was halmashauri hiyo.  Alisema kiwanda hicho kitakuwa ni mali ya Serikali na kipo ndani ya hospitali ya Halmashauri ya Meru Tengeru. 

” Tunatengeneza barako kwa ajili ya watumishi wetu wote wa sekta ya afya kwa vituo vyetu vya afya na zahanati barakoa hizi zitasaidia kuwakinga ili wasipate ugonjwa huu wa Corona 19,” alisema Jerry Muro. 

0172 picha ikionyesha mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akikagua baadhi ya barakoa zilizotengenezwa na kiwanda hicho  Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akigawa baadhi ya barakoa kwa baadhi ya Viongozi wa zahanati za Wilaya yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...