JESHI la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne,watatu wakiwa familia moja kwa tuhuma za kumuuwa kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni na sehemu za siri Baba yao Lumba Nhalima(57).
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha Kasekese wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi wakati marehemu akitoka kunywa pombe na kuelekea nyumbani.

Akithibitisha tukio hilo,Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi Benjamin Kuzaga alisema, siku ya tukio watuhumiwa walimnywesha pombe nyingi marehemu ili ashindwe kujitambua kwa lengo la kumdhuru.

Kwa mujibu wa kamanda Kuzaga ni kwamba,marehemu akiwa njiani kurudi nyumbani alikutana na watuhumiwa hao ambao ni Sali Lumba(32) Jonas Lumba(28) na Paulo Lumba(19) na mtu mwingine ambaye alikuwa anakunywa naye pombe marehemu aliyetambulika kwa  Thomas Malongo(54)

Kuzaga alisema, baada ya uchunguzi jeshi la Polisi limebaini kuwa, kabla ya kifo  chake marehemu alikuwa akilalamika kuwa watoto wake wan ne ambao ni wa mke mkubwa aitwaye Wande Mabuki(46)wanataka kumuuwa ili  yeye na watoto warithi mali zake.

Hata hivyo Kuzaga alisema, chanzo cha kifo hicho kinahusishwa nan a Imani za kishirikina pampja na tamaa za kurithi mali, kwa hiyo Jeshi la Polisi linaendelea kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wengine waliohusika katika tukio hilo.

Aidha Kamanda Kuzaga amesema, baada ya mahojiano ya kina watuhumiwa hao wanne wamekiri kuhusika kupanda njama na kufanikisha mauaji.

“jeshi la polisi linatoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Katavi kuachana na dhana potofu za kujipatia kipato kwa njia ambazo si halali ikiwemo njia za kishirikina” alisema Kamanda Kuzaga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...