JESHI LA POLISI (M) MWANZA CHINI YA KAMISHENI YA USHIRIKISHWAJI WA UMMA KATIKA KUZUIA VITENDO VYA UHALIFU KWA KUTUMIA MFUMO WA ULINZI SHIRIKISHI KWA LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA 4, IKIWA NI PAMOJA NA KUKAMATA INJINI ZA BOTI (BOAT) ZA AINA MBALIMBALI 13, HIYO IKIWA NI SEHEMU YA MWENDELEZO WA OPARESHENI KALI DHIDI YA WAHALIFU KATIKA ZIWA VICTORIA.
HUSUSANI VISIWA VYA JUMA, GEMBALE NA ZILAGULA, VILIVYOPO WILAYA YA SENGEREMA, AMBAPO WALIKAMATWA WATUHUMIWA WANNE AMBAO NI;-1. FILBERT KIPARA @ LWASA, MIAKA 56, MUHA, MKAZI WA NYAMANOLO, 2.BONIFACE AUGUSTINO @ BANDIA, MIAKA 42, MUHA, MKAZI WA KISIWA CHA IZILAGULA, 3.PAUL MARTIN @ DANGOTE, MIAKA 34, MJALUO, MKAZI WA KISIWA CHA IZILAGULA NA 4.JOHH ENOS MAGASHI, MIAKA 57, MSUKUMA, MVUVI, MKAZI WA KISIWA CHA GEMBALE, KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA MAKOSA YA UNYANG’ANYI NA WIZI WA INJINI ZA BOAT INJINE HIZO NI KAMA IFUATAVYO;-
INJINI BOAT 4 AINA YA YAMAHA AMBAPO ENGINE BOAT 2 ZINA HORSE POWER 15 NA NYINGINE ZINA HORSE POWER 9.9.
INGINE BOATS 9 AMBAZO BADO HAZIJAWEZA KUTAMBULIKA AINA NA UWEZO WAKE, HATA HIVYO INJINI ZOTE 13 ZIMEFUTWA SERIAL NAMBA ZAKE.
JESHI LA POLISI PIA LINAENDELEANA KUDHIBITI WATU WOTE WANAOKIUKA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI NA KUWATAKA WALE WOTE WALIOKUTWA NA MAKOSA KULIPA FAINI ZAO NAKUENDELEA KUHESHIMU SHERIA HIZO. KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MINNE JANUARI HADI APRILI 2020 TUMEFANIKIWA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI KWA 78% IKILINGANISHWA NA KIPINDI KAMA HICHO MWAKA 2019 AMBAPO AJALI ZILIPUNGUA KWA 44%.
PIA YAMEKAMATWA MAKOSA 39,329 NA KULIPA FEDHA KIASI CHA TSHS 1,179,870,000/=,(BILIONI MOJA MILIONI MIAMOJA SABINI NA TISA LAKI NANE NA SABINI ELFU TU), MADENI YALIYUOSANYWA KUTOKANA NA MAKOSA YA NYUMA 40,567 YALIKUWA NA THAMANI YA TSHS 1,467,285,000/=(BILIONI MOJA MILIONI MIA NNE SITINI NA SABA LAKI MBILI THEMANINI NA TANO ELFU TU)
HATA HIVYO JESHI LA POLISI (M) MWANZA CHINI YA KAMISHENI YA USHIRIKISHWAJI WA UMMA KATIKA KUZUIA VITENDO VYA UHALIFU KWA KUTUMIA MFUMO WA ULINZI SHIRIKISHI KWA NAMNA YA KIPEKEE LINATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA KAMPUNI YA MWANZA HUDUMA KWA KUTOA MAGURUDUMU 100 MAPYA YA GARI (TYRES), KWA AJILI YA KUBORESHA MIFUMO YA KIUSALAMA IKIWEMO HUDUMA ZA DORIA NA MISAKO KWA KUTUMIA MAGARI AMBAYO KWA SEHEMU KUBWA YALIONESHA KUWA KATIKA HALI AMBAYO SIO NZURI KWA UFANISI NA USALAMA KWA WANAO YATUMIA.
MSAADA HUU WA MAGURUDUMU UTAKUWA NI CHACHU KWA ASKARI POLISI KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA KIAPO CHAO LAKINI PIA SHERIA, TARATIBU NA KANUNI VITAZINGATIWA ILI KUBORESHA HALI YA USALAMA KATIKA MKOA WA MWANZA .
IMETOLEWA NA:-
Muliro J. MULIRO-ACP
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
13 MEI 2020.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...