Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ULRICH MATEI leo tarehe 04.05.2020 majira ya saa 05:00 Alfajiri amefanya ukaguzi wa
kushtukiza wa Mabasi ya Abiria yanayofanya safari kwenda mikoa mbalimbali kabla
ya kuanza safari kwa lengo la kuangalia usalama wa vyombo hivyo vya usafiri
pamoja na kujiridhisha na usimamizi na utekelezaji wa maelekezo yake kwa
wakaguzi wa magari waliopo Stendi Kuu.
Katika
ukaguzi huo alikuta Mabasi matatu ya abiria yenye namba za usajili T.619 CQV aina ya Scania Mali ya Kampuni ya
Isamilo Express linalofanya safari kati Mbeya – Mwanza ambalo tari zake
zilikuwa zimeisha na lilikuwa na tatizo kwenye mfumo wa breki, Basi namba T.420 DNM aina ya Toyota Coaster Mali ya
Kampuni ya Amazon Tour Express linalofanya safari kati ya Mbeya –
Sumbawanga tairi zake zilikuwa zimeisha na Basi namba T.606 DLQ aina ya Euchre Mali ya Kampuni ya Gitu Express pia tairi
zake zilikuwa zimeisha.
Kutokana
na matatizo hayo, Kamanda MATEI
alizuia mabasi hayo kuendelea na safari hadi yatakapofanyiwa marekebisho ikiwa
ni pamoja na kuwekewa tairi mpya. Uongozi wa Kampuni ya Isamilo Express ulileta
basi jingine la kampuni hiyo na abiria kuhamia kwenye basi hilo na kuanza
safari, pia basi la kampuni ya Amazon Tour Express lilibadilishwa tairi na
kuruhusiwa kuendelea na safari.
Aidha
Kamanda MATEI amekagua usalama wa
abiria kabla ya kuanza safari hasa kipindi hiki cha uwepo wa ugonjwa wa Homa
Kali ya Mapafu [COVID 19] na kuwataka Madereva, Abiria na Uongozi wa Stendi Kuu
ya Mabasi Mbeya kuhakikisha kila mmoja anafuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi
Wakuu wa Nchi pamoja na Wizara ya Afya hususani kuvaa barakoa, kunawa mikono
kwa maji tiririka yenye sabuni au vitakasa mikono [Sanitizer] ili kujikinga na
maambukizi ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu.
Aidha
Kamanda MATEI ametoa wito kwa
wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhakikisha wanafanya matengenezo mara kwa mara
ya vyombo hivyo kabla na baada ya safari ili kujiridhisha juu ya usalama wake.
Pia amewataka abiria kutoa taarifa za mienendo ya mabasi hayo kwa Jeshi la
Polisi kupitia namba za simu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya madereva
wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI -SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...