
Hukumu hiyo imetolewa jana Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mshtakiwa huyo kukiri shtaka lake na hivyo kutiwa hatiani.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Simba amesema amezingatia maombi ya mshtakiwa kuwa anategemewa na familia na hivyo, mahakama imemuhukumu kulipa faini ya Sh. Milioni moja au kwenda jela miaka mitatu.
Hata hivyo, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo , Wakili wa Serikali, Ngwijo Godfrey akisaidiana na Sitta Shija, aliiomba mahakama itoe adhabu kali dhidi mshtakiwa huyo ili fundisho kwa wengine.
Katika kesi ya msingi, mshtakiwa anadaiwa kuingia nchini bila kuwa na kibali katika kesi ya jinai namba 76/2020.
Anadaiwa kutenda kosa hilo, Mei 12, 2020 mtaa wa Ohio wilaya ya Ilala, ambapo alikutwa hati ya kusafiria ilisha muda wake na hivyo kuishi nchini bila kuwa na kibali huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...