Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
JO
Ann mbunifu wa nywele amebadilisha ndege iliyotelekezwa katika moja ya
karakana huko Greenwood kwa kutengeneza vyumba vitatu, sehemu ya
kupumzika na jiko.
Ann aliibadilisha ndege hiyo ya abiria Boeing 727 na kuiita jina la Rais wa Marekani Donald Trump.
Makazi hayo yanapatikana huko Benoit, Mississippi karibu na uwanja wa ndege wa Greenwood.
Imeelezwa
kuwa Ann alianzisha makazi hayo mapya aliyoyaita "Nyumba bora
ulimwenguni" mara baada ya makazi yake kukumbwa na dhoruba ya barafu.
Ndege
hiyo yenye urefu wa mita 42 ilianza kufanya kazi kuanzia Mei 1968 hadi
Septemba 1993 huku ikielezwa kuea iligharimu dola 2000 kuinunua na
inakadiriwa marekebisho yake yatagharimu zaidi dola 30,000.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...