Mkurugenzi wa Shirika la Childbirth Survival
International (CSI),nchini Tanzania Stella Mpanda(katikati) akitoa msaada wa
vyakula kwa moja ya wakazi wa Kata ya Mazizini jijini Dar es Salaam leo Mei 2
mwaka 2020.Msaada huo ni kwa ajili ya kuziwezesha kaya za watu wasiojiweza
katika kipindi hiki cha janga la Corona.Kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya
Mtaa Mazizini Mussa Komba.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mazizini Mussa
Komba akikabidhi msaada wa vyakula kwa mwaanchi wa Kata ya Mazizini jijini Dar
es Salaam.Msaada huo umetolewa na CSI kwa ajili ya wananchi wasiojiweza
kiuchumi.Wengine wanaoshuhudia ni watumishi wa CSI wakiongozwa na Mkurugenzi
wao Stella Mpanda(watatu kushoto).
Mkurugenzi wa Shirika la Childbirth Survival
International (CSI),nchini Tanzania Stella Mpanda(wapili kushoto) na Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa ya Mazizini jijini Dar es Salaam Mussa Komba wakimkabidhi
msaada wa vyakula mwananchi wa kata hiyo leo Mei 2 mwaka 2020.
Mkazi wa Mazizini jijini Dar es Salaam(
aliyebeba mtoto) akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali
ya Mtaa Kata ya Mazizini Mussa Komba.Wengine wanaoshuhudia ni watumishi wa
Shirika la CSI.
Watumishi wa Shirila la CSI wakiongozwa na
Mkurugenzi wao Stella Mpanda wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kutoa msaada wa
vyakula kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya kuwasika mkono katika kipindi hiki cha
janga la Corona.
Mkurugenzi wa Shirika la Childbirth Survival
International (CSI),nchini Tanzania Stella Mpanda(kushoto) akielezea umuhimu wa
jamii ya Watanzania kuhakikisha wanafuata maelekezo yanayotolewa na Serikali
katika kukabiliana na janga la Corona.
Mmoja ya wananchi wa Kata ya Mazizini jijini Dar
es Salaam akinawa maji kabla ya kuingia kwenye ofisi za Shirika la CSI kwa
ajili ya kupata msaada wa vyakula.
Mkurugenzi wa Shirika la Childbirth Survival
International (CSI),nchini Tanzania Stella Mpanda(kushoto) akikabidhi msaada
kwa mwananchi leo Mei 2 mwaka 2020.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KATIKA kukabiliana na changamoto zilizopo nchini
kutokana na uwepo wa janga la Corona Shirika la kimataifa la Childbirth Survival International
(CSI),limetoa msaada wa vyakula , sukari na sabuni kwa kaya zaidi ya 50 za watu
wasiojiweza zinazoishi Kata ya Mazizini Ukonga jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa CSI ni kwamba kutokana na uwepo wa
virusi vya Corona nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania wananchi wanapita
kwenye wakati mgumu, hivyo kwa kutambua hilo wameamua kutoa msaada huo kwa
jamii ya watanzania na hasa yenye uhitaji.
Akizungumza leo Mei 2, 2020 jijini Dar es Salaam
wakati wa utoaji wa msaada huo, Mkurugenzi wa CSI nchini Tanzania Stella Mpanda
amesema wamekuwa wakihusika kusaidia wanawake,wajawazito
na vijana lakini kwa wakati huu wa Corora kupitia ofisi zao zilizoko Marekani
na za hapa nchini Tanzania wameamua kuwakarimu wanananchi wasiojiweza wa kata
ya Mazizini.
"Wananchi hawa ambao hawana uwezo wamekuwa
wakipata changamoto kwenye utafutaji riziki na kipindi hiki cha Corona hali zao
kiuchumi ni mbaya zaidi, hivyo shirika letu limeamua kuwasaidia vyakula vya
aina mbalimbali, sukari na sabuni.
"Kwa hiyo tumeona tuwasaidie kwa kiasi, kwa
kuchukua hiki kidogo ambacho tunacho, kwa siku ya leo tumesaidia zaidi ya kaya
50 na wote hao tumewapa mchele, sukari maharage,unga na mche wa sabuni,hivyo ambavyo tumetoa kwetu
tunaona ndio jambo la msingi. Tutaendelea kusaidia jamii yenye uhitaji kadri
tutalavyojaaliwa kupitia wadau wetu mbalimbali"amesema Mpanda.
Kuhusu Corona, Mpanda amesema pamoja na kutoa
msaada huo, wametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wananchi kuendelea kuchukua
tahadhari zinatolewa na Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari.
Mpanda amesema kuwa kasi ya maambukizi ya Corona
kwa sasa ni kubwa, hivyo ni muhimu wananchi kuendelea kuvaa barakoa, kunawa
maji tiririka na sababu , kupaka vitakasa mikono huku akisisitiza ugonjwa huo
ni halisia na unaua.
"Kwa hali ilivyo ni lazima tuchukue
tahadhari na kubwa zaidi tujitahidi kuepuka mikusanyiko ambayo haina ulazima na
ni bora kwa wale ambao hawana sababu ya kutoka nje ya nyumba zao wakabaki
nyumbani tu, hii itasaidia kupunguza kasi ya maambukizi,"amesema Mpanda.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kata ya Mazizini
Ukonga jijini Dar es Salaam Mussa Komba ametoa shukrani kwa niaba ya wananchi
kutokana na msaada huo huku akisisitiza umuhimu wa wananchi kufuata maelekezo
ambayo yanatolewa na Wizara ya Afya na ili kukabliana na ugonjwa huo kila mtu
kwa nafasi yake anatakiwa kuchukua hatua ikiwemo ya kufuata maelekezo ya
watalaam wa afya.
Mmoja ya wananchi aliyepata msaada huo Habiba
Tawaqal amesema anashukuru CSI kutoa msaada huo ambao umewafariji na kubwa
zaidi umekuja wakati mauafaka na kuhusu Corona ni vema jamii kutambua umuhimu
wa kuvaa barakoa kwani ugonjwa huo ni hatari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...