Mwenyekiti wa Programu ya Tunandoto   wa pili  kushoto  Godlisten Koka  akimkabithi Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Monduli Anderson Ulaya    miche 500 ya miti kutoka katika uongozi  wa Programu  yao  inayotekelezwa kwa kushirikiana  na  kanisa la Free Pentecostal church of Tanzania-FPCT Monduli juzi (picha na WOINDE SHIZZA)
 
 
Na Woinde Shizza,MONDULI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Stephen Anderson Ulaya jana amepokea miche 500 ya miti kutoka katika uongozi Wa Programu inayojulikana kwa jina la Tunandoto,Programu inatekelezwa kwa kushirikiana na kanisa la Free Pentecostal church of Tanzania-FPCT Monduli.

Makabidhiano ya miche hiyo yamefanyika katika viunga vya Halmashauri ya wilaya ya Monduli Akizungumza kabla ya kumkaribisha mwenyekiti wa Programu hiyo ,kiongozi wa kanisa la FPCT-Monduli mchungaji Julius Rukyaa alisema kuwa dhamira ya kanisa hilo ni yakuhakikisha kwamba linashirikiana na Serikali katika jitihada za upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi

Alibainisha kuwa ugawaji wa miche ya miti kwa ajili ya kuboresha mazingira ni moja ya shughuli zinazofanywa na Tunandoto Programu ,ambapo wamejipanga zaidi kugawa miti Katika sehemu ambazo Zina ukame zaidi ili wananchi wapande na waweze kukabiliana na ukame

Alisema Shughuli nyingine zinazofanywa na programu hiyo ni pamoja na mafunzo ya ujasiriamali,kilimo hifadhi,utunzaji wa mazingira na ufugaji wa nyuki,Lengo likiwa ni kuwainua wananchi kiuchumi,ambapo aliongeza kuwa tangia Mradi ulipoanza zaidi ya wanachi zaidi 1000 ikiwepo wanachi wa Monduli wameshapata mafunzo tajwa na kaya zaidi 100 wameanza kufaidi mafunzo.

Akipokea miche hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Monduli Stephen Anderson Ulaya ameushukuru uongozi wa Programu ya Tunandoto kwa kuipatia wilaya miche hiyo 500 ya miti,yenye Lengo la kusaidia kuboresha mazingira katika wilaya ya Monduli.

“aliwashukuru Viongozi wa kanisa Wakishirina na Programu ya Tunandoto kwa Mchango mkubwa wa Kutoa Miche ya Miti 500 ili kurudisha uoto wa asili ambao umeharibiwa na Mabadiliko ya Tabia nchi na kuhakikisha tunalo jukumu la kurudisha uoto wa asili ili kupunguza athari za Mabadiliko ya tabia nchi “alibainisha Ulaya .

Pia ameshukuru kwa utoaji elimu kwa Wananchi na ameomba Kama kutatokea fursa ya kuwasaidia wananchi na Kutoa mafunzo. Washirikiane katika kutatua changamoto za Maisha na kuwajenga kiuchumi.

Aliwataka wadau wengine kuendelea kushirikiana na uongozi wa wilaya katika zoezi zima la upandaji miti ili kutimiza adhma ya serikali yakukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya nchi kupitia zoezi la upandaji wa miti.

Baada ya kupokea miche hiyo ya miti Mkurugenzi mtendaji ameikabidhi miche hiyo kwa meneja wa wakala wa misitu (TFS)na kuwataka wahakikishe inapandwa na kutunzwa kikamilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...