Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt. Sophia Mlote na Mwenyekiti wa baraza la wadau wa maziwa Catherine Joseph wakinywa maziwa ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha kila mtu kunjwa maziwa katika kipindi hiki za wiki ya maziwa kitakachofanyika tamati jijini Dodoma Juni 1, 2020.
Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt. Sophia Mlote na Mwenyekiti wa baraza la wadau wa maziwa, Catherine Joseph wakigonganisha glasi katika wiki ya kunywa maziwa ikiwa kila mtu anatakiwa kunywa maziwa lita 54 kwa mwaka.
Mwenyekiti wa bodi ya maziwa, Catherine Joseph akizungumza na waandishi wa habari jini Dar es Salaam leo. Mwaka huu wiki ya maziwa itaadhimishwa Kieletroniki kwaajili ya kujikinga na Virusi vya Corona (COVID-19).
Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt. Sophia Mlote akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua wiki ya maziwa itakayoadhimishwa jijini Dodoma kuanzia Mei 28 na kuhutimishwa Juni 1,2020. Kushoto ni Mwenyekiti wa baraza la wadau wa maziwa, Catherine Joseph.
Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
WANANCHI waaswa kunywa maziwa yaliyosindikwa kwaajili ya usalama na ubora wake hii ni kuelekea wiki ya kunywa maziwa ambapo kila kifikapo Juni 1 kila mwaka shirika la chakula duniani (FAO) liliinisha kuwa siku ya maziwa dunia.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa baraza la wadau wa maziwa, Catherine Joseph wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni kuelekea wiki ya kunywa maziwa itakayo hitimishwa jijini Dodoma Juni 1,2020. Amesema kuwa Matumizi ya maziwa ni borakwa rika zote na yanafaida katika kujenga afya ya mwili wa binadamu.
Amesema kuwa katika kuadhimish wiki ya maziwa wananchi watajifunza teknolojia malimali zinazotumika katika malisho, uzalishaji, ukamuaji na usindikaji wa maziwa ili kuongeza ubora wa maziwa na bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.
Licha ya hilo Catherine amesema kuwa jamii itaunganishwa na wadau wa tasnia ya maziwa ikiwa pamoja na wafugaji, wasindikaji pamoja na wafanyabiashara wa mitambo na vifaa mbalimbali vinavyotumika katika usindikaji wa maziwa hapa nchini kwaajili ya kubadilishana uzoefu.
Kauli mbiu mwaka huu "Wiki ya maziwa 2020 chagua viongozi bora kwa maendeleo ya Tasnia ya maziwa"
Ikiwa mwaka huu takwimu za uzalishaji maziwa zinaonyesha kuwa lita za maziwa zaidi ya lita bilioni 3 ambazo ni ongezeko la asilimia 4 ingawa kwa mwaka 2019 maziwa yalizalishwa lita bilioni 2.7.
Kwa upande wake Msajili wa Bodi ya Maziwa Dkt. Sophia Mlote amesema kuwa tukio la maadhimisho ya wiki ya maziwa itafanyika kwa njia ya kiletroniki kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari matangazo yakirushwa moja kwa moja.
Hivyo amewaasa wananchi kufatilia vyombo vya habari ili kuadhimisha pamoja siku ya maziwa duniani huku tukijikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona (COVID-19) ambapo virusi hivyo vimeikumba dunia nzima.
"Uboreshwaji katika unywaji wa maziwa na bidhaa zake na soko la maziwa bodi ya Maziwa Tanzania inashirikiana na wizara ya mifugo na uvuvi pamoja na wadau mbalimbali katika kuleta ubora zaidi wa bidhaa za maziwa." Amesema Sophia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...