Leo tarehe 11/05/2020 Mkuu wa Wilaya ya Monduli Mheshimiwa Iddi Hassani Kimanta amepokea vifaa kinga kwajili ya ugonjwa covid_19.
Mkuu wa wilaya amepokea Ndoo kumi za kunawia mikono pamoja na Vitakasa mikono Chupa kumi kutoka kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania -FPCT kupitia mradi wake wa Tunandoto Tanzania Programu.
Akikabidhi msaada huo Mchungaji wa Kanisa hilo hapa Monduli Mch.Wilbert Mollel akifuatana na Mratibu wa mradi ndg.Lomayani Laizer amesema kuwa Kanisa limeona kuwa Lina wajibu mkubwa kuunga mkono Serikali katika kupambana na ugonjwa huu mbaya wa Covid_19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
Katika makabidhiano haya Mheshimiwa hayo Mkuu wa wilaya alikuwa pamoja na Mganga mkuu wa wilaya Dr.Titus Mmasi ambapo amewahimiza wananchi wa Monduli kufuata Tahadhari zote ambazo zinatolewa na watalamu wa afya ikiwemo mikusanyiko isiyo ya lazima na kunawa mikono.
-MONDULI BILA CORONA INAWEZEKANA
-TUENDELEE KUCHUKUA TAHADHARI KWA KUFATA KANUNI ZA AFYA
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Monduli
11/05/2020
Jumatatu
Na Elifuraha Kaburu.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...