Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi
akiwapongeza wauguzi wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani.

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi MNH-Mloganzila Sr. Redemptha Matindi akifafanua jinsi taaluma ya uuguzi inavyofanya kazi.

Baadhi ya wauguzi waliohudhuria katika maadhimisho hayo.

Afisa Muuguzi wa MNH-Mloganzila Bw. Amos Mtemi akiendelea kutoa huduma kwa mgonjwa wakati wa maadhimisho hayo.

Wauguzi wakiwa wamewasha mishamaa ishara ya upendo, uvumilivu, heshima, ukarimu na kujitoa katika taaluma hiyo.

Dkt. Magandi na Sr. Matindi wakikata keki.

Sr. Matindi akimkabidhi kipande cha keki mmoja wa wauguzi katika maadhimisho hayo.
…………………………………………………………………….
Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila katika kumbukizi ya siku ya wauguzi duniani
imewapongeza wauguzi kwa kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa lengo
ikiwa ni kuonyesha kuwa inatambua na kuthamini mchango wa wauguzi katika
kuihudumia jamii.
Maadhimisho hayo hufanyika Mei 12, kila mwaka ambapo mwaka huu yana kauli mbiu isemayo “Wauguzi sauti inayoongoza kwa dunia yenye Afya”.
Akizungumza wakati wa maadhimisho
hayo, Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa
Muhimbili-Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi amewapongeza wauguzi kwa kuwa
mstari wa mbele kwa kutoa huduma bora za afya huku wakizingatia kanuni
na taratibu zilizowekwa na taaluma hiyo.
“Nawapongeza sana kwa kumbukizi
ya miaka 200 ya taaluma ya uuguzi tunatambua na kuthamini mchango wenu
kwa kuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma huku mkijali utu, taaluma
hii ni ya muhimu sana na mnaweza kuwa mmejionea jinsi hospitali
inavyoendelea kufadhili masomo kwa wauguzi mbalimbali wanaojiendeleza
ili kuboresha utoaji huduma katika hospitali yetu” amesema Dkt. Magandi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
wa Huduma za Uuguzi wa MNH-Mloganzila, Sr. Redemptha Matindi amewaeleza
wauguzi kuwa taaluma ya uuguzi ni taaluma inayohitaji upendo, utu,
heshima, kujali na kujitoa ili kuwapatia wagonjwa huduma stahiki bila
kujali uwezo au uofauti wa kipato.
Katika kuadhimisha siku hii
wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila walikata keki na
kuwasha mishumaa ikiwa ni alama ya kuwakumbusha kuendelea kutoa huduma
kwa upendo, ukarimu, uvumilivu na kujali utu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...