Kamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (kushoto)
akikabidhi zawadi ya Keki kwa Mkurugenzi wa Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa
wa Dodoma, Stanley Mahundo (kulia) ikiwa ni ishara ya kuwapongeza
Wauguzi kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pamoja na keki hiyo, Dkt. Fatma
alikabidhi pia sabuni kwa ajili ya Wauguzi hao kuzitumia kunawia mikono
kwa ajili ya kujikinga na Korona.

Mkuu wa Kituo cha kutunza Watoto na Wazee cha Home of Joy and Love
kilichopo Hombolo, Dodoma, Sister Fidence MC (kulia) akimuonesha
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma
Rashid Khalfani (katikati) mabweni wanayokaa Watoto alipotembelea
kituo hicho Mei 11, 2020. Kushoto ni Afisa wa THBUB, Fides Shayo.

Sister Fidence, MC, Mkuu wa Kituo cha kutunza Watoto na Wazee cha Home of Joy and Love
Kilichopo Hombolo jijini Dodoma akimtembeza Kamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (kulia)
kumuonesha maeneo mbalimbali ya kituo hicho Mei 11, 2020. Ziara hiyo ya
Kamishna ilikuwa na lengo la kutoa elimu ya haki ya afya ili
kuwahamasisha kuendelea kuzingatia maelekezo yanayotolewa ya kujikinga
na maradhi ya Korona. Kushoto ni Afisa wa THBUB, Fides Shayo.

Kamishna wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Dkt. Fatma Rashid Khalfani (Kulia)
akiongea na Mkurugenzi wa Wauguzi katika Hospitali ya Mkoa Dodoma,
Stanley Mahundo alipomtembelea Hospitali hiyo kwa lengo la kuwapongeza
Wauguzi kuelekea maadhimisho ya Siku ya wauguzi duniani
inayosheherekewa Mei 12 ya kila Mwaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...