Alhaj Issihaka Kibodya muwakilishi wa Watanzania waishio marekani na ustadh Sefu Jongo toka Masjid Noor barabara ya 9 hapa Dodoma walifanya juhudi ya kuwasiliana na gereza la Isanga hapa Dodoma na kupata mahitaji ya wafungwa wa kiislaam na taratibu ya kupeleka dawa, vifaa tiba, sabuni na dawa za mswaki.
Pichani ustadh Sefu Jongo kushoto, Alhaj Issihaka Kibodya katikati wakimkabidhi mkuu wa Gereza la Isanga afande SSP Fredrick Wambura na pembeni yake ni Dr. Pantaleo mganga Mkuu wa Gereza la Isanga.
Tuendelee kujitolea na kuwakumbuka ndugu zetu wasiojiweza na wafungwa.
taarifa hii imetolewa na kitengo cha mawasiliano Masjid Noor barabara ya 9 Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...