MSANII maarufu wa vichekesho nchini, Idriss Sultan na Mwenzake Innocent Maiga, wamefikishwa katika Mahakama ya Ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mawili ya makosa ya mtandao.

Katika shtaka la kwanza Idriss anadaiwa kushindwa kufanya usajili wa  laini ya simu ambayo ilikuwa inamilikwa na mtu mwingine na Maiga anakabiliwa na kosa la kushindwa kutoa taarifa juu ya mabadiliko ya laini ya simu.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa na wakili wa serikali Mwandamizi Wankyo Simon akisaidiana na mawakili wa serikali Batlida Mushi na Estazia Wilson imedai washtakiwa walitenda makosa hayo katika nyakati tofauti tofauti kati ya Desemba Mosi mwaka jana na Mei 19, 2020 huko Mbezi beach ndani ya Wilaya ya Kinondoni.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Rashid Chaungu imedaiwa, Sikh hiyo Mshtakiwa Idriss alitumia laini ya simu iliyokuwa katika usajili wa mtu airways airways Innocent Maiga bila ya kutoa taarifa kwa mtoa leseni.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa Maiga akiwa mmiliki wa laini hiyo ya simu alishindwa kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo inayotumiwa na Idriss kwa mtoa leseni.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana ambayo yaliliwataka lila mmoja kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho na poa wametakiwa kuwasilisha vitambulisho vyao mahakama I hapo. Aidha wametakiwa kusaini bondi ya Sh. Milionin15 lila mmoja.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi dhidi ya kesi hiyo umekamilika na imeahirishwa hadi Juni 9 mwaka huu kwa ajili ya washtakiwa kuja kusomewa maelezo ya awali tayari kwa kuanza usikilizwaji wa kesi. 

Mshtakiwa Idriss ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya  yaliyowekwa na mahakama na mwenzake Maiga ameshindwa kutimiza masharti kwa sababu mmoja kati ya wadhamini wake anakabiliwa na kesi ya jinai mahakamani hapo

Katika kesi hiyo washtakiwa hao wanatetewa na wakili Gebra Kambole baada ya wakili mwenzake Benedict Ishabakaki kuondolewa kuwakilisha washtakiwa kwa sababu atatumika kama shahidi wa upade wa Jamhuri kwa sababu  alishuhudia mshitakiwa wake akichukuliwa maelezo ya onyo Polisi.
Wakili Wankyo amedai wakili Ishabakaki hawezi kuendelea.na uwakilishi huku pia akiwa ni shahidi wa Jamuhuri tunaomba asiwe kuruhusiwa kuendel2a na uwakilishi.

"Nilishuhudia mteja wangu akitoa maelezo hivyo naomba nijitoe katika kesi hii",  amejibu wakili Ishabakaki.

Kesi imeahirishwa hadi Juni 9, 2020.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...