Na Zainab Nyamka, Michuzi TV
Kampuni
ya michezo ya kubahatisha Parimatch imefanya maboresho makubwa katika
tovuti yao ya kubashiri, ambayo kwa sasa itawawezesha wateja wao na
watanzania kiujumla wanaopenda kubashiri kujumuika pamoja.
Wateja
wa Parimatch watacheza kwa pamoja michezo yote ya Simulated Reality
League, E-Sports, masumbwi na soka ambayo inatarajiwa kurejea Mei 16
ikianza na Ligi ya Ujerumani ‘Bundesliga,’ kwa kutumia intaneti kidogo.
Hayo
yamesemwa na Meneja Mkuu wa Parimatch Tanzania, Tumaini Maligana
wakati alipokuwa akizundua rasmi jukwaa hilo la kubashiri mtandaoni
kupitia www.parimatch.co.tz
na kusema kwamba imekuwa ni desturi yao kusikiliza maoni ya wateja wao
kila mara na kuamua kuyafanyia uamuzi ili kusudi waweze kuwapatia kitu
kilichokuwa bora wateja wao ambao hutumia muda wao ziada kujiburudisha
akili zao na Parimatch.
“Tumefanya
mabadiliko mazuri, tumerekebisha mambo mengi. Katika kipindi hiki
ambapo watu wengi wapo nyumbani tumeona ni vyema kuwapa njia mbadala ya
kupata burudani, kukaa ndani ni suala jema lakini pia kwa afya ya akili
burudani ina nafasi yake. Wateja wetu wote watatumia taarifa zao za
zamani kuingia www.parimatch.co.tz na wataiona Platform yetu mpya.
Aidha,
Maligana amesema katika maboresho hayo ambayo Parimatch imefanya katika
kipindi hiki, yataweza kuwaruhusu watumiaji wa simu za android kuitumia
kwa njia ya application kwa urahisi na ufanisi mkubwa zaidi.
Pamoja
na hayo, Maligana pia aliwasisitizia wadau wa Parimatch kuendelea
kufurahia kucheza Virtual game na michezo mingine mbalimbali kupitia
tovuti yao ambayo itaweza kukuburudisha na kusisimua katika kipindi hiki
cha Corona na hususani tukisubiri ligi nyingine zirejee.
Kwa upande mwingine.
Parimatch
imeendelea kuwa mkombozi mkubwa kwenye soko la michezo ya kubahatisha
ndani ya nchi na nje ya mipaka ya Tanzania, kwa kuweza kutoa betting
zenye ubora, malipo ya papo hapo kwa haraka baada tu ya mchezo
kumalizika bila ya kusahau huduma ya wateja bora ndani ya masaa 24 siku 7
za wiki kwa takribani miaka 25 hadi hivi sasa.
Meneja Mkuu wa Parimatch Tanzania Tumaini Maligana
Вот тут есть обзор и рейтинг букмекерских контор, например букмекерская контора Пари Матч с официальной лицензией и полностью легальная.
ReplyDelete