Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imefanya Uboreshaji wa Sheria na Mamlaka ya Udhibiti ya Usafiri Majini, Kuboresha shughuli za uokoaji, Miundombinu ya Bandari na Uboreshaji wa Mafunzo na Utoaji vyeti vya Mabaharia ikiwa ni hatua muhimu za kuimarisha usalama wa usafiri majini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe jijini Dodoma wakati akieleza mikakati iliyochukuliwa na Serikali katika kuimarisha usalama wa usafiri majini nchini ikiwa ni miaka 24 tangu kuzama kwa Meli ya MV Bukoba katika Ziwa Victoria.

Waziri Kamwelwe amesema serikali ya awamu ya tano imejipambanua katika kuboresha usafiri kwa njia ya maji katika maziwa Makuu kwa kufanya miradi mbalimbali ambayo inajumuisha ukarabati wa meli mbili katika Ziwa Victoria ambazo ni MV Victoria na MV Butiama ambazo sasa zitaitwa New MV Victoria Hapa Kazi Tu na New MV Butiama Hapa Kazi Tu.

Amesema kuna miradi ya ujenzi wa Chelezo kubwa na ujenzi wa meli mpya kubwa katika Bandari ya Mwanza Kusini jambo ambalo litaongeza safari kwenye Ziwa hilo kubwa Afrika Mashariki.

Kuhusu uboreshaji wa Sheria na mamlaka ya udhibiti ya usafiri majini, Mhandisi Kamwelwe amesema serikali ilibadilisha sheria ya 'Maritime Transport Ordinance of 1967' na kutunga sheria ya 'Merchant Shipping Act, 2003 (MSA 2003)" ili kusimamia usafiri wa majini.

" Katika kuimarisha utekelezaji huo, Serikali kupitia Wizara yetu sekta ya Uchukuzi imetengeneza kanuni 27 ili kuwezesha mamlaka inayodhibiti usalama wa usafiri wa maji ni kusimamia utekelezaji wa sheria hii.

Serikali imeendelea kuimarisha usimamizi wa usalama wa usafiri majini kwa kuhakikisha uwepo wa Ofisi na Wakaguzi wa meli was TASAC katika mikoa yote inayopakana na Maziwa Makuu ambapo usimamizi huo unahusisha, Kuidhinisha michoro ya meli na kusimamia ujenzi wa meli mpya, kufanya kaguzi za kawaida na kushtukiza na kuzuia meli zisizo salama," Amesema Mhandisi Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe amesema katika kuboresha shughuli za utafutaji na uokoaji, Serikali imeendelea kuwekeza katika kuimarisha shughuli za utafutaji na uokoaji hii ni pamoja na kuanzisha Kituo cha uokoaji na utafutaji cha Dar es Salaam.

Amesema serikali kwa kushirikiana na Shirika la Bahari duniani imejenga Kituo cha kuratibu shughuli za utafutaji na uokoaji katika Bandari ya Dar es Salaam na Kituo hiko kitasimamiwa na TASAC na kufanya kazi saa 24 kwa juma zima.

Aidha kupitia Mamlaka ya Usimamizi ya Bandari (TPA) Serikali imeimarisha miundombinu ya Bandari katika maziwa Makuu na Bahari ya Hindi ili kuwezesha bandari kuwa salama na zenye ufanisi zaidi. Juhudi hizo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa bandari ya Ziwa Victoria na nyingine za maziwa makuu na pia upanuzi wa Bandari za Bahari ya Hindi.

" Kupitia uboreshaji wa sheria ya TASAC, serikali imeimarisha usimamizi wa mafunzo na utoaji vyeti vya mabaharia chini ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kwa mujibu wa Itifaki ya Kimataifa. Vyeti hivyo vinavyotolewa na TASAC vinatambuliwa Kimataifa na hivyo kuwawezesha mabaharia wetu kufanya kazi katika meli yoyote duniani," Amesema Waziri Kamwelwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma kuhusiana na mikakati ambayo Serikali imechukua kuimarisha usafiri wa majini nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...