Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuhakikisha wanafunzi wa kidato cha sita wanaorejea mashuleni wanakua salama, Serikali imewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kuandaa miundombinu itakayowezesha wanafunzi hao wanachukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Naibu Katibu Ofisi ya Rais-Tamisemi anaeyeshughulikia elimu, Gerald Mweli alipofanya ziara ya kukagua shule zenye wanafunzi wa kidato cha Sita Mkoani Dodoma ili kuangalia maandalizi ya kuwapokea wanafunzi hao ambao watarejea Mei 30 na kuanzia masomo Juni 1 mwaka huu.

Mweli amewataka viongozi hao kushirikiana na uongozi wa shule hizo za serikali na binafsi kuhakikisha vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo kama ndoo za kunawia maji tiririka na sabuni zinakuepo, Vitakasa mikono na Barakoa lakini pia elimu itolewe kwao.

Amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutenga wataalamu wa afya ambao watakua wanazihudumia shule hizo katika kipindi hiki huku akiwataka wakuu wa shule kuwajenga kisaikolojia wanafunzi na kuwaondoa hofu juu ya ugonjwa huo.

" Wakuu wa shule hakikisheni mnawajenga wanafunzi kisaikolojia na kuwaondolea hofu ili waweze kuzingatia masomo na akili yao kuweza kurudi katika hali ya kawaida lakini pia chukueni tahadhari kama ambavyo Wizara ya Afya imekua ikisisitiza.

Suala la mita moja madarasani, Bwenini na kwenye mikusanyiko mingine pia mlizingatie, tunaamini watoto watakua katika mikono salama kwa kushirikiana na viongozi wenu wa Halmashauri, " Amesema Mweli.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Dodoma, Amani Mfaume amesema kuwa uongozi wake umechukua tahadhari zote  zilizotolewa na wizara ya afya na kusisitiza kuwa watatumia wiki moja kukamilisha silabasi  kwa masomo ya kemia na fizikia na kuwa wiki tatu kabla ya mtihani zitatumika kufanya marejeo ya masomo.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Msalato, Neema Maro amesema wamejipanga kuwapokea wanafunzi wao watakaporejea na tayari wameshaanza kushona barakoa zitakazoendana na idadi yao pamoja na kununua kipimo cha Joto ili kuwapima wanafunzi kila mara.
Naibu Katibu Ofisi ya Rais-Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli (kulia) akiwa na viongozi wengine wakikagua mabomba ambayo yanatiririsha maji kwa ajili ya kunawia katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato jijini Dodoma.

 Naibu Katibu Ofisi ya Rais-Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli akikagua miundombinu ya maji katika Shule ya Sekondari Dodoma.
 Naibu Katibu Ofisi ya Rais-Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato kujionea namna walivyojiandaa kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita Mei 30 mwaka huu.
 Naibu Katibu Ofisi ya Rais-Tamisemi anayeshughulikia Elimu, Gerald Mweli (katikati) akiwa kwenye ukaguzi Sekondari ya Dodoma ikiwa ni maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha sita Mei 30, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...