Waziri Ummy Mwalimu akipokea mfano
wa hundi wenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 kwa ajili ya ununuzi wa
vifaa tiba na vifaa kinga kutoka Anglogold Ashanti pamoja na Geita Gold
Mining Limited(GGML)

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipokea mataki ya maji kutoka kwa
Wamiliki wa Malori nchini ambayo yatapelekwa kwenye mipaka yote
nchini.Kulia ni Mwenyekiti wa TPSF Bi.Angelina Ngalula

Baadhi ya watumishi wa Shirika la
Maendeleo la Petrol Tanzania (TPDC) wakikabidhi hundi kwa Waziri wa Afya
kwa ajili ya mapambano ya kukabiliana na COVIDI-19

Waziri Ummy Mwalimu akiongea mara
baada ya kupokea msaada wa vifaa kinga,tiba na fedha kwa ajili ya
mapambano ya kukabiliana na COVID-19 kutoka kwa wanachama wa sekta
binafsi zipatazo kumi

Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF
Geofrey Simbeye akiongea wakati wa makabidhiano hayo ambapo alisema
taasisi yao iko bega kwa bega na Serikali katika mapambano hayo

Mwakilishi wa chama cha
wanamitindo nchini Mustafa Hassanali akiongea wakati wa kukabidhi vifaa
kinga kutoka kwa wanamitindo mbalimbali nchini

Mwakilishi kutoka TBL Group
Georgia Mutagahywa akiongea wakati akikabidhi vifaa kinga ambavyo
vitatumika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...