Na Woinde Shizza,ARUSHA
Chama Cha wafanyabiashara ( TCCIA)Mkoa wa Arusha kwa
kushirikiana na Trade Mark East Africa na TRIAS kimegawa vifaa kinga
vyenye thamani ya sh,mil. 4 kwenye masoko matatu katika jiji la Arusha
kama njia Moja wapo ya kupambana na maambikizo ya ugonjwa hatari wa
Corona na kuunga mkono jitihada za serikali dhidi ya ugonjwa huo.
Akikabidhi
vifaa hivyo zikiwemo ndoo za maji ya kutiririka,vitakasa mikono na
Barakao ,mwenyekiti wa TCCIA ,Wolter Maeda aliwataka wafanyabiashara
katika masoko hayo kuhakikisha wanajikinga na Corona kwa kutumia vifaa
hivyo.
Aliwakumbusha
wafanyabiashara hao kuhakikisha wafanyabiashara zao katika mazingira
salama ,ikiwemo kuosha mikono yao kwa sabuni kukaa umbali wa mita moja
na kuvaa barakoa ili kujikinga na janga hilo .
"Nipende
kuwasihi wafanyabiashara na kuwaambia ugonjwa huu upo na unaua kweli
kweli ni vyema kuchukuwa taadhari na kuacha kupuuzia ushauri unaotolewa
na idara ya afya ,hapa tu nikiangalia kunawafanyabiashara hawajavaa
barakoa ,nimeona hawanawi mikono sasa niwaombe msifanye mzaa kwenye
ugonjwa huu chukuweni taadhari "alibainisha Maeda
Naye
Afisa Maendeleo ya Biashara wa TCCIA,Charles Makoi alisema kuwa masoko
yaliyonufaika na msaada huo ni Kilombero,Samunge(Krokon) na Soko kuu
ambapo wanufaika wa mpango huo ni wafanyabiashara wadogo(Machinga),Mama
ntilie na wauzaji wa mbogambona na matunda.
Aliwasihi
wananchi kuendelea kupeana elimu wao kwa wao nila kuopa na kuoneana
aibu ili kuweza kuendelea kuwanusuru wale ambao wapo majumbani na wale
ambao bado hawajaelewa au elimu haijawafikia ya kujikinga na ugonjwa huu
wa Corona pamoja na wale ambao wamesikia lakini bado wanapuuzia .
Hata
hivyo aliahidi kuendelea kusaidia zaidi katika maeneo mengine yenye
mkusanyiko kuhakikisha wananchi wanadhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...