Mke wa Mbunge wa Bariadi, Mhe.
Andrew Chenge, Mama Christina Chenge (wa nne kushoto) akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya viongozi mara baada ya kukabidhi msaada wa
kompyuta tano na printa moja kwaShule ya sekondari Simiyu kwa niaba ya
Mbunge huyo, Mei 04, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka (kushoto) akimkabidhi Afisa Elimu Halmashauri ya Mji wa
Bariadi nakala ya mkakati wa maalum wa kuwawezesha wanafunzi kujisomea
wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi
vya Corona, ambao umezinduliwa Mei 04, 2020 katika shule ya Sekondari
Simiyu Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda sambamba na mapokezi ya msaada
wa kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew
Chenge.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu,Mwl.
Ernest Hinju akitoa maelezo juu ya mkakati maalum wa mkoa wa
kuwawezesha wanafunzi kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari
dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona, ambao umezinduliwa Mei 04,
2020 katika shule ya Sekondari Simiyu Mjini Bariadi uzinduzi huo ulienda
sambamba na mapokezi ya msaada wa kompyuta tano na printa kutoka kwa
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji wa idara ya
elimu katika uzinduzi wa mkakati maalum wa kuwawezesha wanafunzi
kujisomea wakati wa likizo ya dharura ya tahadhari dhidi ya maambukizi
ya Virusi vya Corona, ambao umezinduliwa Mei 04, 2020 katika shule ya
Sekondari Simiyu Mjini Bariadi sambamba na mapokezi ya msaada wa
kompyuta tano na printa kutoka kwa Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew
Chenge.
-Mke wa Mbunge wa Bariadi, Mhe.
Andrew Chenge, Mama Christina Chenge (wa pili kulia) akikabidhi moja ya
kompyuta tano na printa zilizotolewa na Mbunge huyo kwa Shule ya
Sekondari Simiyu, kulia ni Mkuu wa Shule hiyo, Mwl Paul Susu akipokea
msaada huo Mei 04, 2020; kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bariadi, Juliana Mahongo.
********************************
Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkoa wa Simiyu
umezindua mpango mkakati wa kuwawezesha wanafunzi wa shule za Msingi na
Sekondari kusoma katika kipindi hiki cha likizo ya dharula ya tahadhari
ya ugonjwa wa homa ya mapafu ( COVID 19) inayosababishwa na Virusi
vya Corona.
Akizindua
mkakati huo, Mei 04, 2020 katika Shule ya Sekondari Simiyu Mjini
Bariadi, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa
mkakati huo utawasaidia wanafunzi kupata masomo wakiwa nyumbani kutoka
kwa walimu wao huku ukiwa na malengo makuu manne yatakayoifanya Simiyu
iendelee kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa.
” Malengo
makuu ya mkakati huu ni kumwezesha mwanafunzi kuendelea kujifunza,walimu
kuwa na mawasiliano ya kitaaluma na wanafunzi wao, wazazi kufanya
ufuatiliaji wa taaluma kwa watoto wao pamoja na watoto(wanafunzi)
kutulia nyumbani wakijisomea kipindi hiki cha likizo ambayo wako
nyumbani; tahadhari zote za maambukizi ya Virusi vya Corona
zitazingatiwa, “alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka
amewataka wazazi na walezi kuwahimiza wanafunzi kutulia nyumba
kujisomea na kufuatilia vipindi vya masomo mbalimbali vinavyorushwa
kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini, huku akisisitiza maelekezo
yote yanayotolewa na wataalam wa afya na viongozi juu ya tahadhari ya
maambukizi ya Virusi vya Corona yazingatiwe wakati wa kujisomea.
Afisa Elimu
wa Mkoa wa Simiyu, Mwl Ernest Hinju amesema Mkoa utaendelea kufanya
mawasiliano na wazazi ili siku tatu baada ya shule kufunguliwa wanafunzi
wapewe mitihani ili kuwapima.
Katika hatua
nyingine mbunge wa jimbo la Bariadi, Mhe. Andrew Chenge ametoa msaada
wa kompyuta tano na printa kwa Shule ya sekondari Simiyu kutoka mamlaka
ya mawasiliano kwa wote ambazo zimekabidhiwa na Mjumbe wa Baraza la UWT
Taifa, Christina Chenge (mke wa mbunge huyo) kwa niaba ya mbunge.
Akikabidhi
kompyuta hizo, Mama Christina Chenge amesema mbunge ametoa msaada huo
na ametoa wito kuwa kompyuta hizo zitumike kwa kazi na malengo
yaliyokusudiwa ili mkoa wa Simiyu uendelee kufanya vizuri katika sekta
ya elimu.
Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amemshukuru Mhe. Chenge kwa msaada huo na
misaada mingine ambayo amekuwa akiitoa kwa shule ya Sekondari Simiyu na
shule nyingine ikiwemo saruji na mabati kwa ajili ya ujenzi wa madarasa
na mabweni na kusisitiza msaada huo kutumika kama ulivyokusudiwa.
Akiongea mara
baada ya makabidhiano ya msaada huo, Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe.
Festo Kiswaga amesema kuwa hategemei kuona shule hiyo (Simiyu sekondari)
iliyokabidhiwa vifaa hivyo kupata wanafunzi wenye daraja sifuri kwani
tayari wana walimu na vifaa vya kutosha sambamba na madarasa ya
kutosha.
Naye mkuu wa
shule ya sekondari Simiyu, Paul Susu amemshukuru Mhe. Chenge kwa
kutambua uhitaji walionao kwani utawasaidia katika kutekeleza shughuli
zao za ufundishaji huku akiongeza kuwa pamoja na kuwa shule ya Simiyu
ndio imekabidhiwa shule nyingine zitanufaika pia kwa kuwa wanafanya kazi
kwa ushirikiano na shule nyingine.
Nao baadhi ya
walimu wa shule hiyo akiwemo Dorine Bella na John Mogela wamesema kuwa
ujio wa kompyuta hizo utakuwa chachu ya kurahisisha ufundishaji na
kutekeleza mkakati wa mkoa wa wanafunzi kusoma katika kipindi hiki cha
ugonjwa wa homa ya mapafu na baada ya ugonjwa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...