MSANII anayekimbiza kwenye tasnia ya uchekeshaji nchini, Abdallah Sultan a.k.a Dullivan amezindua rasmi shindano la "Asante fans".
Dullivan
amesema kuwa kutokana na kupokelewa kwake vizuri na mashabiki zake
ameamua kurudisha fadhila kwa mashabiki zake kupitia shindano hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari amesema kuwa vigezo vya kushiriki kwenye
shindano hilo ni kumfwatilia kwenye mitandao yake ya kijamii kwa njia ya
kuchangia ujumbe mfupi na kuwa-tag watu wa tano kwenye picha ambazo
atakuwa anatuma kwenye mtandao wake wa Instagram na kupata mshindi.
"Shindano
hilo litakuwa kwa kila wiki kwa njia ya simu na hii nimeamuwa kufanya
hivyo kwa lengo la kurudisha asante kwa mashabiki zangu kwa mafanikio
ambayo nimepata tangu nimeanza kazi zangu za uchekeshaji"
Aliongezea kuwa kwa wiki hii mshindi atapata kiasi cha fedha laki 5 kwa watu wa tano na kwamba shindano hilo halichagui ni kwa watu wote.
Hata
hivyo Dullivan ameeleza kuwa jamii inayomzunguka bado inaendelea kumpa
nguvu hasa mama yake mzazi tangu ameanza kazi hiyo mpaka Sasa hivyo
hategemei kukatishwa tamaa kutokana na kuvaa uhusika wa kike (mama
chogo) kuanzia mavazi,lafudhi pamoja na madoido .
''Wakati
mwingine mama yangu mzazi mwenyewe ananichagulia mavazi Kama vijora na
ananishauri kabisa vitanipendeza kutokana na rangi zake hivyo naona ndio
baraka ananimwagia na anachukulia Kama kazi zingine tu ndio maana
nafanikiwa napata kazi nyingi na ndio maana napata na mimi nguvu ya
kurudisha fadhila kwa mashabiki,".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...