Na Farida Saidy,Morogoro

Chama cha Watu wenye ualbino ( TAS) kimeiomba serikali kuangalia upya sera na  miongozo   katika sekta ya  afya kuwasidia watu wenye ualbino katika upatikanaji wa vifaa kinga  ikiwemo mafuta maalumu ya kujipaka ,kama ilivyo  katika upatikanaji wa dawa za kufumpaza virusi vya Ukimwi ARV zinavyotolewa bure katika vituo vya afya na zahanati.

Kauri hiyo imetolewa mkoani Morogoro na katibu wa  Tas Taifa Musaa Kabimba  katika kliniki ya ngozi  kwa watu wenye ualbino, ambapo alisema anatambua  mchango wa Serikali  katika kuwasaidi kundi hilo lakini changamoto ni upatikanaji wa  vifaa kinga kwani kumekua na gharama kubwa ukilinganisha na maisha yao ambapo mafuta ya kujipata ili kujikinga  na Saratani yanauzwa kuanzia elfu 35 Hadi elfu 40 jambo ambalo wengine wanashindwa kumudu bei hizo na kuiomba serikali kuandaa utaratibu wa kuwapatia bure kama makundi megine.

Kwa upande wake Afisa Afya wa Tas Taifa Bwana Mohamed Chanzi alisema saratani ya ngozi ni miungonimwa magojnwa yanawapa  changamoto  watu wenye ualbino  ambao asilimia kubwa ya wagonjwa wanaopatika na Sratani ya Ngozi wanakua wameathirika kwa kiwango kikubwa 

Naye daktari bingwa magonjwa ya ngozi amesema    katika kuwasaidia watu wenye viashiria vya dalili vya saratani ya ngozi wanachomelewa na mionzi ili kupunguza uwezekano wa kupata Saratani huku afisa ustawi wa Jamii Mratibu wa watu wenye ulemavu na Wazee mansipaa ya Morogoor Rehema Malimi kaeleza jitihada wanazofanya katika kusaidia kundi hilo Ni pamoja na kulipatia elimu jinsi ya kujinginga wasipate maradhi

Nao baadhi ya Baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ualbino wamekishukuru chama hicho pamoja na serikali katika kuwahakikishaia usalama watoto wao ukilinganisha na kipindi cha nyuma walikua wakiishi kwa hofu wakihofiausalama wa maisha yao.

Siki ya watu wenye ualbino ufanyika kila ifikapao juni 13 kila mwaka  lengo kutoa elimu kwa jamii kuhusu watu wenye ualbino ambao mwaka huu kutokana na Ugonjwa wa Covid 19 haitafanyika  katika makundi. 
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...