Na Karama Kenyunko,Michuzi TV

MAHAKAMA ya Hakimu Kisutu imewahukumu wafanyabiashara wanne wakazi wa Dar es Salaam kulipa faini ya shilingi  500,000 kila mmoja  ama kifungo cha miaka mitatu jela  kwa kosa la kukutwa na madini tofauti tofauti yenye uzito  gram 131 yenye thamani ya zaidi shilingi milioni 100  kinyume na sheria.

Wafanyabiashara hao Noah Mmasanga, Richard  Boniface, Ally Said na Mosses Mbojo ambapo wamehukumiwa kulipa faini hiyo baada ya kufika makubaliano na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini DPP ya kukiri makosa yaliyokuwa yakiwakabili.

Hukumu hiyo imesomwa leo mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mwandamizi Vicky Mwaikambo baada ya kujiridhisha na vielelezo vilivyo wasilishwa mahakamani hapo na upande wa Mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali mwandamizi Renatus Mkude.

Akiwasilisha hoja ya upande wa Jamuhuri Wakili  Rwnatus Mkude alidai vielelezo vilivyokamatwa ni pamoja na Madini aina ya Tanzanite, Ruby, Vocanic Glass gram 131 pamoja na kadi ya gari aina ya Toyota Raum yenye namba za usajili T 716 DJP.

Baada ya Mahakama kujiridhisha na vielelezo hivyo, Wakili Mkude akaiomba mahakama hiyo kutaifisha madini hayo pamoja na gari lililotumika kusafirisha madini hayo nakulipa faini kama walivyofikia makubaliano na DPP.

Hata hivyo baada ya kusikiliza hoja za pande zote,  Hakimu Mwandamizi Mwaikambo aliamuru nyara hizo kutaifishwa kuwa Mali ya serikali nakuwataka washitakiwa kulipa faini kwa mujibu wa sheria ama kifungo cha miaka mitatu jela.

Washtakiwa hao hakuwa na pingamizi yoyote juu ya maamuzi hayo baada ya mahakama kuwatia hatiani  na kukiri kosa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...