Bunduki ya kivita aina ya AK47 ambayo imekamatwa wilayani Ngorongoro na Jeshi la polisi wakishirikiana pamoja na kikosi cha ujangili kanda ya Ziwa huko Oloshoo Kata ya Enguserosambu picha Zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Sehemu ya risasi zilizokutwa kwenye magazine ya bunduki hiyo baada ya msako mkali wilayani Ngorongoro

Askari wa kikosi kazi cha Jeshi la Polisi akijaribu Silaha hiyo mbele ya waandishi wa habari kabla kamanda wa Jeshi hilo hajaongea nao leo jijini hapa

Kamanda Shana akiwa na maafisa wa Jeshi hilo wakija kuongea na vyombo vya habari mapema leo jijini hapa .

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akiongea na vyombo vya habari havipo pichani kuelezea matukio mawili ya uhalifu na wahalifu



Waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari mkoani Arusha na nchini wakifuatilia matukio wakati kamanda wa Jeshi la Polisi akizungumza nao makao makuu ya jeshi hilo jijini Arusha picha zote na Ahmeid Mahmoud Arusha











Kamanda Shana akiwaonyesha waandishi wa habari silaha iliyokamatwa haipo pichani leo jijini Arusha.

Kamanda Shana akijaribu silaha hiyo kuonyesha inavyofanyakazi mbele ya waandishi wa habari leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha


Na Ahmeid Mahmoud

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha huko kwenye kitongoji cha Oloshoo kata ya Enguserosambu Tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wamefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya AK 47 yenye namba H 49 ikiwa na risasi 12 iliyokuwa njiani kufanya uhalifu kwenye Mbuga za wanyama.

Aidha kwa muktadha huo Mapambano dhidi ya matukio ya uhalifu na wahalifu ambapo kwa kipindi hichi wahalifu wengi hudhani jeshi la polisi limelala hivyo niwahakikishie hatujalala na tunaendelea kufanya misako na opereseheni mbalimbali iwe wakati wa mvua Jua Tope au Masika Baridi au kiangazi kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutenda uhalifu.

Akiongea na vyombo vya habari mkoani hapa kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana alisema kuwa kikosi hicho kabambe baada ya kupewa taarifa fiche kuwa kuna watu 4 wawili watanzania na wakenya wawili wameonekana maeneo ya Mpakani wakiwa wanajipanga kuwinda wanyama adimu kwenye mbuga zetu muhimu.

Kwa mujibu wa Kamanda Shana baada ya kupata taarifa hizo kikosi kazi chenye askari machachari wazalendo na wenye weledi wa hali ya juu waliendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini juu ya taarifa hiyo na tarehe 10.6.2020 tulifanya msako mkali katika kijiji hicho kuwatafu wahalifu hao.

Alisema kuwa katika msako huo wahalifu wawili walikamatwa wakiwa na silaha moja ya kivita aina ya AK 47na risasi zake 12 ndani ya magazine ambao majina yao tunayahifadhi kwa ajili ya uchunguzi huku jeshi hilo likiendelea kuwatafuta watuhumiwa wawili waliokimbia nchi jirani ya Kenya.

Aidha jeshi la polisi linawasaka wahalifu hao kujisalimisha mara moja kituo chochote cha polisi kwani wasipofanya hivyo tutalazimika kutumia nguvu kubwa kuwatafuta ili hatua kali za kisheria zichukuliwe.

Kamanda Shana akatumia fursa hiyo kuendelea kuwashukuru wananchi ambao wameendelea kutoa taarifa mbalimbali za uhalifu na wahalifu huku akiwataka kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuwafichua wale wote wenye nia ovu ili kumaliza uhalifu kwenye mkoa wetu.

Amebainisha kuwa Jeshi hilo mkoani hapa linaahidi litatoa donge nono kwa yeyote atakaye toa taarifa zitakazo fanikisha kuwakamata wahalifu wanaojihusisha na Uwindaji haramu ,Ujambazi ,na uhalifu wa aina yeyote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...