NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA VIJIJINI
NAIBU
Waziri Wa Maji ,Jumaa Aweso ameiagiza RUWASA na DAWASA Mkoani Pwani
,kuongeza uzalishaji wa maji na kusimamia mradi wa maji wa Kipangege
Kibaha ,ili wananchi wanaondokane na tatizo la kupata maji kwa mgao
,kwani wananchi hao wamechoshwa na maji ya kudunduliza .
Aidha
ameielekeza ,RUWASA Mkoani hapo ,kuhakikisha wanamuondoa msimamizi wa
mradi wa maji wa Kipangege, Kibaha na kuurudisha mradi mikononi mwa
Jumuiya ya watumiaji ili kuondoa kero ya upatikanaji wa maji ya uhakika
na kuchota maji kwa sh .150-200 kwa ndoo badala ya sh.100 iliyopangwa.
Aweso
alitoa maagizo hayo ,wakati alipofanya ziara ya siku moja ,Kibaha
Vijijini kufuatilia maelekezo aliyoyatoa yafanyiwe kazi katika mradi wa
maji Kipangege ambao aliutembelea mwishoni mwa mwaka jana .
Alieleza
,adhma ya Serikali ya awamu ya tano ,chini ya Rais dkt.John Magufuli ni
kumtua mama ndoo kichwani hivyo juhudi ziendelee ili kutimiza adhma
hiyo .
":Nilipata ombi la
kuja hapa kutoka kwa mbunge wenu Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa , mwezi
Desemba 2019 nilifika na nilitoa maagizo RUWASA Mkoa ,wilaya na DAWASA
kuufuatilia mradi na kuhakikisha maji yanatoka "
"Nashukuru
maji yalianza kutoka toka January mwaka huu lakini tatizo bado ni mgao
unaosababisha kero pamoja na usimamizi mbovu kwa mkandarasi
aliyekabidhiwa na wananchi awasimamie ,ni bora mradi urudi kwa wananchi
waendeshe wenyewe, kwakuwa ni kwa ajili yao ,wanufaike nao na sio
kumnufaisha mtu mmoja " alisisitiza Aweso .
Hata
hivyo ,Aweso alimtaka ofisa ununuzi RUWASA kuharakisha mchakato wa
manunuzi ya vifaa vinavyotakiwa kwenye kuongeza kituo kimoja cha
kuchotea maji ,";kuboresha mradi kwa kujenga mnara na ununuzi wa tanki
la lita 10,000 ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa haraka.
Nae
mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini, Hamoud Jumaa ,alisema Kipangege
ulikuwa na shida ya maji kwa miaka mingi hivyo ujio wa Naibu Waziri huyo
umewanufaisha wakazi hao .
Jumaa
aliishukuru serikali ,RUWASA ,na DAWASA kwa juhudi yao katika
upatikanaji wa maji kwenye baadhi ya maeneo jimboni hapo ikiwa ni moja
ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi .
Mwenyekiti
wa Kipangege Shomari Jumaa,alieleza wanapata maji kwa mgao ambapo
marekebisho na uboreshaji ukifanyika wataendelea kunufaika na mradi huo .
Meneja
wa RUWASA Mkoa wa Pwani ,Beatrice Kasimbazi alipokea maagizo yote na
kusema watahakikisha wanaupokonya usimamizi wa mradi kwa mkandarasi na
kuukabidhi kwa wananchi.
Alielezea
,ili kuboresha mradi kwa kujenga mnara wa mita 6 na tanki la lita
10,000 na kuongeza kituo kimoja cha kuchotea maji mchakato wa ununuzi wa
vifaa tayari unafanyika na upo mwisho kukamilika .
Kasimbazi
alifafanua ,mradi wa Kipangege ni kati ya miradi 26 mkoani Pwani ,na
Kibaha ni mradi mmoja uliokuwa na changamoto , uliotegemewa kukamilika
2014 ulisuasua na RUWASA ilipoanzishwa ulifanyiwa kazi na kuanza kutoa
maji January 2020 .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...