Na Karama Kenyunko- Michuzi TV

MFANYABIASHARA wa Jijini Dar es Salaam, Poison Batisha (36), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya Uhujumu yenye mashtaka ya kukwepa kodi, kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya zaidi ya sh. Bilioni tatu na utakatishaji fedha.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali Janet Magoha amedai Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janet Mtega kuwa, kati ya Januari Mosi 2012 na May 12, 2020 ndani ya jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa alikwepa kulipa ongezeko la kodi kwa ajili ya biashara zake za Umeme yenye thamani ya sh. 3,010,092,416 mali ya TRA.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo, mshtakiwa Batisha kwa makusudi aliisababishia TRA hasara ya zaidi ya shilling Bilioni Tatu kwa udanganyifu baada ya kuwepa kulipa kodi hiyo kwa TRA.

Katika shtaka la tatu la utakatishaji fedha imedaiwa, Siku na mahali hapo mshtakiwa huyo alijipatia kiasi hicho cha Sh. Bilioni Tatu kwa kukwepa kulipa kodi huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kukwepa kodi.

Hata hivyo, mshtakiwa Batisha hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi. 
 
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 18,2020 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa mshtakiwa amerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...