Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni kwa upande wa Zanzibar Dkt.Omar Abdalla Adam pamoja na watendaji wake wakutana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw.Godfrey Mngereza.

Lengo ni kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizi mbili kwa kuweka mipango ya pamoja ya utendaji kazi katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Katika kikao hiki  taasisi hizi mbili zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja katika maeneo ya kuwajengea uwezo wasanii na wadau wa sanaa katika suala la mikataba, utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vyema katika Mitihani ya kidato cha nne katika masomo ya Muziki, Sanaa za maonyesho na sanaa za ufundi.

Mashirikiano hayo yanalenga kuwaunganisha wasanii na wadau wa sanaa walioko Tanzania Bara na Visiwani.

Kikao hiki kilichofanyika makao makuu ya BASATA jijini Dar Es Salaam ni muendelezo wa vikao vya ushirikiano kati ya BASATA na BASSFU katika kuimarisha ushirikiano wenye tija kwa sekta ya sanaa nchini Tanzania.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...