Na Amiri kilagalila,Njombe
Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe kimeielekeza
taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kuwakamata hadharani na
kuwachukulia hatua wanachma wa Chama hicho wanaochafua taswira ya Chama kwa
kutumia rushwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Mbele ya vyombo vya habari katibu wa siasa na uenezi
CCM mkoa wa Njombe ndugu Erasto Ngole amesema kwa mujibu wa maelekezo ya vikao
vya chama hakuna mwanasiasa ndani ya chama hicho atakayesalimika katika
mchakato huo kwa kutoa rushwa wala kuandaa makundi ya kukirubuni Chama kwani
kinazo taarifa za baadhi ya wanasiasa wa CCM walioanza kujitokeza wakitoa
rushwa
“Tunaielekeza taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa,tungetamani katika mkoa wetu wa Njombe hawa wanaccm wanatuchafua
wangekamatwa mchana hadharani au usiku na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
kama watuhumiwa wengine”alisema Ngole
“Halmashauri kuu ya CCM ya mkoa imetoa maelekezo
kwamba wale wote ambao tumeshabaini wanapita mitaani na kutoa rushwa,hakuna
atakayepenya,hakuna atakayeteuliwa”alisema tena Ngole
Aidha Ngole amesema kuwa kila mwanachama baada ya
kipyengwa kupulizwa hapo julai 17 mwaka huu atakuwa na haki ya kuchukua fomu
kugombea nafasi yoyote lakini anapaswa kujitathimini kabla ya kuchukua fomu
hizo.
Kwa upande wake katibu wa umoja wa vijana wa ccm (UVCCM)
mkoa wa Njombe bwana Amos Kusakula amesema vijana wanapaswa kushiriki
kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwani wanayo nafasi kubwa badala
ya kudhani kuwa wanatengwa.
“Kwa wa takwimu za sense za mwaka 2012 Inaonekana
zaidi ya asilimia 70 ni vijana,sasa kijana lazima ujitambue na uwe tayari kwa
kuwa vijana ni muda wao na wanatakiwa kuonyesha uwezo wao na vipaji vyao”alisema
Kusakula
Wananchi mkoani Njombe wanazungumziaje vitendo vya
rushwa katika chaguzi mbalimbali.
“Kwa kweli wagombea wanaopita na kutoa rushwa kwa
ajili ya kuchaguliwa hao hawako sahihi kwasababu anakuwa hajiamini,shida ni
kwamba wagombea wengi huwa hawajitambui”Alisema Telesia Mgina Mkazi wa Njombe
mjini
Mwezi Oktoba mwaka huu serikali ya Tanzania
inatarajia kuendesha zoezi la uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi watakaohuduma
nafasi ya Udiwani,Ubunge na Rais katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...