Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinautaarifu Umma kuwa, hakuna Mtumishi yeyote aliyehojiwa na TAKUKURU kama ambavyo Gazeti la Uhuru toleo la Ijumaa Juni 26,2020 lilivyoandika.

Gazeti lililokuwa na kichwa cha habari "TAKUKURU yahoji Vigogo TIC, BRELA" liliandika habari kuhusu Wafanyakazi wa TIC kuhojiwa kwa kuhusika na vitendo vya rushwa ya uuzwaji wa ardhi ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro kwa Raia wa China.

Taarifa hiyo si tu haikujitosheleza kwa kutotaja Watumishi waliohojiwa, bali pia  haina ukweli wowote na kwamba TIC haijihusishi na masuala ya uuzwaji ardhi.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kinafanya kazi kwa kuzingatia weledi.

Kituo kinatoa wito kwa Waandishi wa Habari nchini kujiridhisha na habari wanazotoa kuhusu TIC ikiwepo kupata ufafanuzi wa kina wa masuala mbalimbali yahusuyo Uwekezaji, tunafanya kazi muda wote na wakati wote milango ipo wazi.

TIC inaendelea kuheshimu Taaluma ya Habari na Wanahabari wote wa ndani na nje ya Nchi.

Asante!

Latiffah A. Kigoda Afisa Habari na Uhusiano TIC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...