Na Mwandishi Wetu, Singida
TASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushes( TAKUKURU)Mkoa wa Singida inatarajia kuwafikisha kwenye Mahakama ya Wilaya ya Manyoni ,Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Kilimatinde Bahati Ilikunda na mzazi mwenzake Haji Bwegege ambao kwa pamoja wanatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha Sheria namba 15 cha Kuzuia na Kupambana na Rush namba 1 ya mwaka 2007.
Taarifa ya Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha Adili Elinipenda aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Juni 29,2020 amefafanua kuwa
ofisi yake ilipokea taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja (jina lake limehifadhiwa) kuwa Hakimu Bahati Ilikunda wa Mahakama ya Mwanzo ya Kilimatinde wilayani Manyoni aliomba rushwa ya Sh. 350,000 ili atoe upendeleo kwa mtoa taarifa katika shauri la madai namba 03,2020 ambalo lipo mbele yake.
"Tulipata taarifa Juni 28,2020 huko wilayani Manyoni mkoani Singida katika maeneo ya Kituo cha mabasi yaendayo Dodoma ,hivyo ofisi yetu ilimkamata Haji Bwegege ambaye ni mzazi mwenzake Bahati baada ya kupokea rushwa ya Sh. 170,000 ikiwa ni sehmu ya Sh. 350,000 aliyoombwa.
Elinipenda amesema kwenye taarifa hiyo kwamba uchunguzi wa TAKUKURU Mkoa wa Singida umejiridhisha kuwa Haji Bwegege na Bahati wana uhusiano wa kifamilia kwani wanamtoto waliyemzaa pamoja jambo linaloashiria uwezekano wa Hakimu Bahati kumtuma Haji Bwegege katika kupokea rushwa anazoziomba.
"Hata hivyo Ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Singida tunatoa shukrani za dhati kwa Idara ya Mahakama mkoani hapo kwa jinsi wanavyotoa ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya rushwa kuanzia Mahakama ya Mwanzo hadi Mahakama ya Mkoa,"amesema Elinipenda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...