
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi, aliwapitisha katika maeneo kadha na vitengo tofauti katika hospitalini hiyo ili kujionea namna wanavyofanya kazi na kuwahudumia watanzania.
Hata hivyo Maafisa kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini wamefurahishwa na kazi tunazozifanywa na hospitali hiyo katika kutimiza wajibu wao kwa kutoa huduma kwa wanzania.
"Siku zote tunajivunia kuwa na wadau wa aina hii, wanaotutembelea hospitali yetu katika maeneo mengine tunayofanya kazi kwa ajili ya kuunga mkono katika kutoa huduma." Amesema Brenda
Licha ya hilo hospitali ya CCBRT wameshauriwa kuboresha zaidi na zaidi kwa kile wanachokifanya katika jamii ya watanzania.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akizungumza na Maafisa kutoka ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali hapa nchini walipotembelea hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam leo.
Mazungumzo yakiendelea wakati wakitembelea hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...