Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini SACP David Misime imesema kuwa leo 24/06/2020 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amefanya uhamisho kwa baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa ili kuongeza ufanisi na tija katika kazi za Polisi. 

Miongoni mwa waliohamishwa, amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha na aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana amehamishwa kwenda kuwa Afisa Mnadhimu namba moja  katika Shule ya Polisi Moshi.

Pia IGP Sirro, amemhamisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu Bunge, Dodoma ACP Emmanuel Lukula kwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro na nafasi yake inachukuliwa na ACP Andrew Satta ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Makao Makuu ya Polisi Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...