Na Leandra Gabriel, Michuzi TV

SHIRIKA  la Fedha Duniani (IMF) limeidhinisha kutoa msaada wa Dola za kimarekani Million 14. 3 kwa Tanzania na hiyo kupitia kikao cha bodi ya wakurugenzi kilichokaa jana Juni 10.

Kupitia mfuko wake wa kupambana na maafa(CCRT ) IMF imeisamehe Tanzania kiasi cha mkopo cha Dola za kimarekani milioni 14. 3 ambazo zilipaswa kulipwa ndani ya miezi minne ijayo kuanzia sasa mpaka tarehe Oktoba 13, 2020.

Imeelezwa kuwa hiyo ni katika kunusuru uchumi wa Tanzania ulioathirika kutokana na  mlipuko wa Covid 19.

Hata hivyo IMF kupitia mfuko wake huo wa maafa imeahidi kuendelea kuisaidia Tanzania tena kiasi cha Dola za kimarekani Million 25.7 kuanzia Oktoba kutegemeana na uwezo wa mfuko kwa wakati huo.

Ambapo nyongeza hiyo ya mkopo itatolewa kwa miezi, kuanzia Oktoba 14, 2020 mpaka Aprili 13, 2022.

Akiongea Mkurugenzi mtendeji wa wa Mfuko wa Maafa Tao Zhang amesema  kuwa mlipuko wa Covid 19 kwa kiasi umeathiri uchumi wa Tanzania licha ya Mamlaka nchini humo kuendelea kuchukua  hatua mbalimbali katika Kuhakikisha hakuna tokeo la anguko la kiuchumi.

Amesema kuwa mfuko huo wa maafa utatoa rasilimali kwa umma katika kusaidia janga hilo na mamlaka nchini humo zimejitolea kusimamia rasilimali hizo kwa kusimamia rasilimali kwa matumizi yaliyokusudiwa na kwa uwazi zaidi ikiwa ni pamoja na kupitia kaguzi mbalimbali kuhusiana na matumizi yanayohusiana na COVID.

Pia ameshauri kuwa, ili kuweza kukabiliana na hatari iliyobaki ni muhimu kulinda fedha  kwa ajili ya sekta ya afya na matumizi mengine ya kijamii yaliyopewa kipaumbele  katika bajeti ya FY 2020/21 na pia kuhakikisha ukaribu baina ya Shirika la Afya Duniani (WHO,) Mashirika ya kimataifa na wafadhili unadumishwa.

"Kwa kuangalia mbele zaidi marekebisho ya kimuundo ni muhimu katika kujenga uchumi mkubwa  hasa kwa kuangalia makusanyo ikiwemo kodi na matumizi ya serikali pamoja na kuwezesha mitaji kwa wananchi, mazingira ya biashara na uboreshaji wa mikopo inayotolewa na mabenki" ameeleza Tao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...