Katibu Mkuu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Anuary Mgonde(katikati) akizungumza leo Juni 11,2020 jijini Dar es Salaam kuhusu jukwaa hilo kumpongeza Rais Dk.John Magufuli alivyosimama imara katika mapambano dhidi ya Corona.Pia Jukwaa hilo limetoa tamko la kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli ikiwa pamoja na kuhakikisha anashinda kwa kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu mwaka huu.Wengine ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Mkoa wa Kilamanjaro George Madaraka (kushoto) na Mwenyekiti wa jukwaa hilo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Fatuma Kassara(kulia).
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Mkoa wa Kilimanjaro George Madaraka(katikati) akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano huo.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Anuary Mgonde na kulia ni Mwenyekiti wa jukwaa hilo Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Fatuma Kassara.
 
Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Fatuma Kassara(katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu namna ambavyo walimu walioko kwenye jukwaa hilo wanavyoendelea kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli.Kulia ni Katibu Mkuu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Anuary Mgonde na kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Mkoa wa Kilimanjaro George Madaraka.

 
Baadhi ya walimu walioko kwenye Jukwaa hilo la Walimu Wazalendo Tanzania wakipiga makofi kumpongeza Rais Dk.John Magufuli kwa hatua ambazo amezichukualia katika kukabiliana na janga la Corona.Pia wamempongeza Rais Magufuli kwa namna ambavyo ameendelea kuwajali walimu wote kwani hata wakati wa Corona walimu waliendelea kulipwa mishahara na posho licha ya kuwa nyumbani.
 Katibu Mkuu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Anuary Mgonde(katikati) akifafanua jambo wakati wa mkutano ya jukwaa hilo na waandishi wa habari uliofanyia leo Juni 11,2020 jijini Dar es Salaam.Wengine ni viongozi wa ngazi mbalimbali wa jukwaa hilo katika maeneo tofauti.
 Sehemu ya Walimu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania wakifuatilia kwa makini hotuba ya Katibu Mkuu wa jukwaa hilo Anuary Mgonde alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

 
 
*Waeleza Serikali ilivyokuwa inawalipa walimu Sh.biliioni 300 ndani ya miezi mitatu wakati Corona

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

JUKWAA la Waalimu Wazalendo Tanzania limesema linamshukuru na kumpongeza Rais Dk.John Magufuli kwa msimamo wake na ujasiri wake katika maamuzi aliyoyachukua kama hatua za kupambana na COVID- 19 na Watanzania wote ni mashahidi katika hilo.

Limesema katika kukabiliana na Corona hakuna nchi ambayo iliamini zingeweza kufanikiwa lakini baada ya kizisimamia kwa misimamo isiyoyumba nchi zote sasa zimevutiwa na kuiga hatua zilezile ambazo Rais Magufuli alizichukua na ambazo kama taifa tulizipitia.

Akizungumza leo Juni 11,2020 jijini Dar es Salaam,Katibu Mkuu wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania Anuary Mgonde amefafanua Rais Magufuli alichukua hatua sahihi ambazo licha ya kubezwa na mataifa ya nje, taasisi za kimataifa na hata watanzania wasiokuwa wazalendo kwa taifa lao, hatua hizo zimefanikiwa na zimezaa matunda kwa kuokoa maisha ya watanzania, uchumi wa Taifa letu na kuzidi kuiongezea imani nchi nje ya mipaka ya Taifa.

Amesema hatua ambazo Rais alizichukua ni kutoruhusu watu wazuiwe kuendelea na kazi zao na badala yake wakae majumbani."Hivi kwa hali zetu tuzuwie watu kufanya kazi zao kwa mwezi mmoja tu hakuna mtanzania akaeweza kumudu maisha yake."

Ameongeza mengine ambayo Rais alisimama imara ni kutofunga mipaka, kukataa kufunga nyumba za ibada na kuruhusu watu wamuombe Mungu ili atuepushe maradhi hayo, kuitisha maombi ya kitaifa ya siku tatu pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maradhi haya kwa wananchi kwa ujumla."Mtakumbuka kuwa siku moja baada ya Tanzania kuripoti kesi ya kwanza ya maambukizi ya Corona yaani Machi 16,2020 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa tangazo la Serikali la kufunga shule zote nchini kuanzia awali hadi Chuo Kikuu ili kuwanusuru vijana wetu na watoto wasipate maambukizi ya Covid-19.

"Katika kipindi chote hicho ambacho shule zilikuwa zimefungwa na kusimama kwa masomo, Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli iliendelea kutulipa walimu mishahara na posho kama kawaida tena kwa wakati ule kama vile ilivyokuwa wakati wa ratiba zetu za kazi.Kitendo cha Serikali kulipa mishahara pamoja na posho watumishi zaidi ya 266,905 waliosimama kazi, miezi mitatu mfululizo tena kuwalipa kwa wakati bila kuchelewa au kupitisha tarehe, ni jambo kubwa na linalostahili shukurani za hali ya juu sana,"amesema Mgonde.

Amesisitiza upo usemi wa Kiswahili unasema mnyonge muoneeni haki yake mpeni , hivyo Rasi

Magufuli aliweza kuyafanya hayo katika kipindi ambacho nchi ipo kwenye taharuki kubwa ya maradhi ya vita vya kutetea na kulinda uchumi wake, katika kipindi ambacho kampuni, biashara na taasisi mbalimbali zinafungwa na katika kipindi ambacho nchi nyingine zinapunguza wafanya kazi na kusitisha malipo yao.

"Serikali ya Rais Magufuli iliidhinisha kiasi cha Sh.bilioni 300 kwa mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu mfululizo za kutulipa mishahara na posho katika kipindi ambacho dunia ipo kwenye vita na hofu ya kushuka kwa uchumi wake, huu ni ujasiri na upendo mkubwa, ubinadamu uliopitiliza na huruma ya hali

ya juu."Jukwaa la Waalimu Wazalendo Tanzania tunamshukuru na kumpongeza Raisi wetu kwa upendo huu kwa walimu na tunapenda kumhakikishia yeye na Serikali ya Awamu ya Tano anayoiongoza kuwa waalimu wa Tanzania tutaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa vitendo kama sehemu ya kuenzi mchango wa kihistoria wa walimu katika jenzi wa taifa letu.

"Jukwaa la Walimu Wazalendo Tanzania tunapenda kutoa mwito kwa makundi mbalimbali ya jamii, taasisi za dini, wanamichezo, watumishi wa kada zote na watanzania kwa ujumla tuendelee kumtia

moyo Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya awamu ya awamu ya tano walau

kwa kuthamini na kuunga mkono juhudi zake katika kujenga na kulinda uchumi wa nchi,"amesema.

Pia amesema Serikali imefanya makubwa katika kipindi cha muda mfupi mambo ambayo yalikuwa ni ndoto na hayakufanikiwa kwa muda mrefu na wala hatukufikira kama yanaweza kufanyika, ubunifu aliouonyesha Raisi Magufuli katika miradi ya kimkakati inakwenda kutimiza kauli ya msomi na

mwandishi mahiri wa vitabu ndugu Napoleon Hill aliyesemna kuwa “Chochote ambacho akili ya

binadamu inaweza kuunda na kufikiri, inaweza kukikamilisha pia.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Walimu Wazalendo Mkoa wa Kilimanjaro George Madaraka amesema chini ya Rais Magufuli nchi yetu imepata maendeleo makubwa na wao kama walimu wazalendo jukumu lao ni moja tu kuhakikisha Rais Magufuli anashinda kwa kishindo kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea tu baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya afya ambapo Ujenzi wa hospitali za mpya za Wilaya 67. "Tangu mwaka 1961 tulipopata uhuru hadi 2017 tumekuwa na hospitali za Wilaya 77 tu, Katika Mwaka wa fedha 2018/ 2019 Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli ilitenga Sh. Bilion 100.5 na kujenga Hospitali za Wilaya 67 mpya, jumal zimekuwa 144.

"Ujenzi wa Vituo vya afya vipya 400. Tangu 1961 tulipopata uhuru hadi 2016 tulikuwa na vituo vya

afya 115 nchi nzima vevye uwezo wa kufanya upasuaji, katika Mwaka wa fedha 2017/ 2018,2018/2019 Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli imejenga vituo vya afya vipya vevye uwezo wa

kufanya upasuaji 400.Ukweli kuna mambo mengi ya maendeleo ambayo yamefanyika kwenye nyanja zote ndani ya nchi yetu.Katika ujenzi wa miundombinu ya barabara sote ni mashahidi."

Hivyo Madaraka amesema “Muda mzuri wa kupanda mti ni miaka 20 iliyopita, Lakini muda mwingine mzuri wa pili wa kuanda mti ni sasa.” Ameongeza Serikali ya Awamu ya tano imepanda mazuri mengi, hivyo hatuna budi kuyaendeleza na kuyathamini na kwamba Jukwaa la waalimu wazalendo wanatoa ombi watanzania tuthamini mambo mazuri yanayofanywa Serikali kwa kumuombea Rais wetu na viongozi wote Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...