Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
UNAHISI
vipi ukiambiwa kuhusu kifo? ni wazi kuwa wengi hawafurahii kusikia
habari hizo, lakini watu wengi kutoka Tokyo nchini Japan wanafurahi
wakisikia habari kuhusiana na kifo, watakufa vipi? na namna ya kujiandaa
kabla ya kifo.
Tokyo
hufanya sherehe kila mwaka kwa ajili ya kujiandaa na kifo, "Shukatsu
Festival" watu hufundishwa namna ya kujiandaa kwa kifo, "Shakatsu" kwa
wajapani humaanisha kujiandaa kabla ya kufa na maadhimisho hayo
hufanyika kila Desemba 16.
katika
maadhimisho hayo watu hujengewa uelewa wa namna watakavyowaacha
wapendwa wao wakipitiwa na kifo, maadhimisho hayo huambatana na maonesho
mbalimbali yanayohusu kifo na kwa kuweka uhalisia zaidi watu hulala
katika majeneza, wakiwa wamevaa mavazi ya marehemu huku mafunzo ya namna
ya kuanda miili ya wafu yakiendelea.
Wengi
walioshiriki sherehe hizo wamekuwa wakieleza kuwa wanataka kuona mwisho
wao kabla ya kuufikia na wengi wao hulala katika majeneza na kupiga
picha na baadaye huchagua mapambo, maua na kila kitu ambacho wangependa
kitumike katika siku zao za mwisho.
Japan
si nchi yenye watu wengi duniani (watu milioni 126.5 kwa mujibu wa
takwimu za mwaka 2018) bali pia ni moja ya nchi ambayo inaongoza kwa
kuwa kampuni nyingi za mazishi na kumekuwa na washiriki wa kada zote
wakiwemo wazee na vijana katika sherehe hizo.
Imeelezwa
kuwa maonesho hayo yamelenga kuwakumbusha watu kuhusiana na kifo pamoja
na majonzi na huzuni kwa wale wanaoachwa na imeelezwa kuwa maonesho
hayo yamekuwa ni mwongozo bora katika familia hasa kwa kuzingatia safari
ya kifo.
Sherehe hizo
zimekuwa zikiwavuta pia watalii kutoka nje huku kapuni za mazishi nchini
humo zikipata wateja wengi kupitia Shukatsu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...