Charles James, Michuzi TV

JESHI la Polisi Mkoani Dodoma limethibitisha kushambuliwa na kujeruhiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake jijini Dodoma.

Akizungumza na wandishi wa habari leo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amesema taarifa za Mbowe kushambuliwa na watu wasiojulikana walizipata asubuhi ya leo kupitia kwa Mbunge wa Viti Malum wa Chama hicho.

Kamanda Muroto amesema tayari Jeshi la Polisi limeshaanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku akiwaonya watu wanaosambaza taarifa za uongo pamoja na kupiga marufuku mikusanyiko yoyote isiyo halali.

" Tumepata taarifa za kuwepo kwa wanachama wa Chadema waliopanga kukusanyika kwenye ofisi za Chama cha hapa Dodoma, niwaonye kwamba Jeshi la Polisi halitoruhusu mikusanyiko kinyume na sheria na utaratibu.

Lakini pia tumelichukulia tukio hili kama tukio lingine la uhalifu na tayari tumeshaanza uchunguzi wetu.... niwaonye wale wanaotaka kulitumia tukio hili kisiasa," amesema Kamanda Muroto.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwa amelazwa katika hospitali ya DCMCT iliyoko eneo la Ntyuka jijini Dodoma akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kumakia leo nyumbani kwake jijini humo.Pichani kushoto ni Mnadhimu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni (CHADEMA),Mhe, Ester Bulaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...