Mfanyabiashara Mussa Mohamed akiingia katika mahaka ya hakimu Mkazi jijini Dar es Salaam leo.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia mashtaka Mfanyabiashara Mussa Mohamed aliyefikishwa mahakamani hapo leo Juni 23, 2020  akikabiliwa na mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroine.

Hatua hiyo imekuja baada ya Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto kudai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga kuwa upande wa mashtaka hauna nia ya kuendelea kumshitaki Mohamed kwa kosa hilo.

Aliomba mahakama kufuta shauri hilo chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai.

Mapema akisoma mashitaka dhidi ya mshtakiwa huyo, Mitanto alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni 5, mwaka huu maeneo ya kuhifadhi mizigo ya wasafiri jijini Dar es Salaam.

Alidai mshitakiwa alikutwa akisafirishwa dawa za kulevya aina ya heroine zenye gramu 101.71.

Hata hivyo mshitakiwa alikana mashitaka na upande wa mashitaka ulidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kisha wakawasilisha ombi la kumfutia mashtaka.

Hakimu Ruboroga alikubaliana na maombi ya upande wa mashitaka na kuondoa shauri hilo pamoja na kumuachia huru mshitakiwa.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo amekamatwa tena na kupelekwa mahabusu ya mahakamani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...