Muonekano wa hatua iliyofikiwa ya
sehemu ya chini ya meli Mpya ya MV Mwanza “Hapa Kazi Tu” inayojengwa
katika bandari ya Mwanza Kusini, jijini Mwanza. Ujenzi wa Meli hiyo
unatarajiwa kukamilika mapema mwaka 2021 na itagharamu zaidi ya kiasi
cha shilingi bilioni 80.

Mafundi wa Kampuni ya GAS EntecCo
Ltd, Kang Nam Cooperation ya Korea Kusini pamoja na SUMA JKT ya Tanzania
inayojenga meli ya MV Mwanza, wakiendelea na kazi ya ujenzi wa meli
hiyo, inayojengwa jijini Mwanza

Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya
Huduma ya Meli (MSCL), Luteni Kanali Mhandisi Abel Gwanafyo akifafanua
jambo kwa Wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) na Wataalam wa Sekta hiyo,
walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya MV Mwanza ‘Hapa Kazi
Tu”, Ukarabati wa meli ya MV Butiama, MV Viktoria na Ujenzi wa Chelezo,
mkoani Mwanza

Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya
Huduma ya Meli (MSCL), Luteni Kanali Mhandisi Abel Gwanafyo akiwaonesha
wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Uchukuzi) na Wataalam wa Sekta hiyo, mabadiliko yaliyofanywa
kwenye mifumo ya uendeshaji wa meli ya MV Viktoria wakati walipotembelea
maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya MV Mwanza ‘Hapa Kazi Tu”, Ukarabati wa
meli ya MV Butiama na MV Viktoria na Ujenzi wa Chelezo. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Lucas Kambeleje.

Kaimu Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya
Huduma ya Meli (MSCL), Luteni Kanali Mhandisi Abel Gwanafyo, akiwaonesha
wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Uchukuzi) na Wataalam wa Sekta hiyo, sehemu ya kuhifadhia
mizigo katika meli ya MV Viktoria wakati Menejimenti hiyo na wataaalam
walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya MV Mwanza ‘Hapa Kazi
Tu”, Ukarabati wa meli ya MV Butiama na MV Viktoria na Ujenzi wa
Chelezo, mkoani Mwanza.

Luteni Kanali Mhandisi Vitus
Mapunda, akieleza kwa wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) na Wataalam wa Sekta hiyo,
hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa chelezo wakati Menejimenti hiyo na
wataalam walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa Meli mpya MV Mwanza ‘Hapa
Kazi Tu”, Ukarabati wa meli ya MV Butiama na MV Viktoria na Ujenzi wa
Chelezo, mkoani Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...